Yanga Kiboko Aisee Yaandika Historia Mpya, Huku Mayele Akipiga Goli tatu za Nguvu |Shamteeblog.


STRAIKA wa Yanga, Fiston Mayele amepachika mabao matatu 'hat-trick' ya kwanza msimu huu katika Ligi Kuu Bara dhidi ya Singida BS kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa.

Mayele amefunga 'Hat-trick' hiyo dhidi ya Singida siku tatu baada ya mkewe kujifungua mtoto wa kike na kuiwezesha timu yake kuibuka na mabao 4-1.

Yanga imefikisha michezo 47 ya ligi bila kupoteza tangu msimu uliopita na mara ya mwisho ilipoteza dhidi ya Azam April 25, 2021.

Mbali na kuwa ni hat-trick ya kwanza kwenye ligi msimu huu kwa Mayele ni tatu katika mashindano yote msimu huu mbili alitupia Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Zalan FC ya Sudan Kusini.

Mayele amefunga hat-trick hiyo baada ya ukame wa kukaa miezi miwili bila kutikisa nyavu ikiwa ni sawa na mechi tano kwenye ligi.


Beki wa kulia wa Yanga, Kibwana Shomary alitupia bao lake la kwanza msimu huu huku akishuhudiwa Mayele akihusika kwa kutoa asisti.

Nyota wa zamani wa Simba, Meddie Kagere aliendelea kutesa dhidi ya Yanga kwa kuifungia Singida BS bao la kufutia machozi kwenye mchezo huo.

Hii ilikuwa mara ya kwanza kwa Singida BS kucheza mchezo wa ligi kwenye uwanja wa Mkapa tangu ipande Ligi Kuu.

Kwa mara ya kwanza msimu huu, Abutwalib Hamad Mshery aliruhusu bao kwenye ligi ndani ya michezo mitatu aliyocheza.



from Author

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post