CHUO CHA TAIFA CHA UTALII KUENDELEA KUTOA MAFUNZO BORA YA UKARIMU KWA WANAFUNZI WAKE, WADAU WAWEKA MIKAKATI |Shamteeblog.

Na Mwandishi Wetu
CHUO cha Taifa cha Utalii kimesema kinaendelea kinaendelea kuweka jitihada ya kutoa mafunzo bora ya ukarimu kwa wanafunzi ( Hospitality)kwa wanafunzi wanaosoma chuoni hapo kwa lengo la  kusaidia kuongeza idadi ya Watalii  .

Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Utalii CPA Munguabela Kakulima alipokuwa akizingumza kuelekea Kongamano la kuelekea Maadhimisho ya miaka 61 ya Uhuru wa Tanganyika lililoandaliwa na Chuo hicho.

Kongamano hilo limewakutanisha wadau mbalimbali wakiwemo wasomi, wanazuoni, Wanafunzi pamoja na wadau wa sekta ya utalii lengo likiwa kujadiliana kuhusu sekta  ya Utalii kuanzia kipindi kilichopita na kilichopo kwa sasa nakuweka maazimio ya nini kifanyike ili kufikia malengo ya 2025 ya kuendelea kuongeza idadi ya watalii nchini.

CPA Kakulima amesema wakati Taifa likiadhimisha miaka 61 ya Uhuru , jambo kubwa la kujivunia ni mafanikio makubwa yaliyopatikana tangu kipindi  nchi ilipopata uhuru hadi sasa ikiwemo kuongeza kwa idadi ya watalii kutoka nchi mbalimbali duniani wanaokuja kutembelea vivutio vya utalii.“Tumeendelea kushuhudia idadi ya watlii ikiendelea kuongezeka siku hadi siku.”

Kwa Upande wa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Sokoine (SUA) Ernest Mwamwaja pamoja na mambo mengine ameeleza hatua kwa hatua kuhusu sekta ya sekta ya utalii ambayo kwa sasa imekuwa na hiyo inatokana na mifumo iliyopo ya kusimamia na kuendesha sekta ya utalii nchini tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma.

“Tunakumbuka hapo nyuma ni Serikali peke yake ndio ilikuwa inasimamia sekta hii ya utalii lakini kwa sasa kuna hatua kubwa imepigwa na ndio maana unaona kuna kampuni nyingi kubwa zinajihusisha na utalii ya kiwemo ya ndani na nje ya nchi ambayo yameruhusiwa kuwekeza katika sekta hiyo.Aidha kumekuwepo na wadau wengi  ambao wanategemea utalii kuendesha shughuli zao za kiuchumi.“Kwetu haya ni mafanikio makubwa na tunapongeza jitihada zinazoendelea kuwekwa kwenye kuifanya sekta ya utalii kuwa imara zaidi.”

Kongamano hilo limewakutanisha wadau mbalimbali ikiwemo Wanazuoni,Wasomi,Wanafunzi ikiwa ni kujadili hali ya Sekta ya Utalii kuanzia kipindi kilichopita na kilichopo kwa sasa nakuweka maazimio ya nini kifanyike ili kufikia malengo ya 2025. yakuongeza Watalii zaidi.Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Utalii CPA Munguabela Kakulima  akisoma hotuba yake wakati wa kufungua Kongamano la kuelekea Maadhimisho ya miaka 61 ya Uhuru wa Tanganyika lililoandaliwa na Chuo hicho leo jijini Dar es Salaam.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Sokoine (SUA) Ernest Mwamwaja akingumza wakati wa Kongamano la kuelekea Maadhimisho ya miaka 61 ya Uhuru wa Tanganyika lililoandaliwa na Chuo hicho leo jijini Dar es Salaam.Meza kuu 


Sehemu ya wadau wa Chuo hicho  pamoja na Mwanafunzi wakiwa  katika Kongamano la kuelekea Maadhimisho ya miaka 61 ya Uhuru wa Tanganyika lililoandaliwa na Chuo hicho leo jijini Dar es Salaam.



 


By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post