Hospitali China zaelemewa wagonjwa wa Covid -19 |Shamteeblog.

Shirika la afya duniani ( WHO) limesema kuwa kuna uwezekano hospitali nchini China zikaelemewa na wagonjwa wa Uviko 19.

Hii ni baada ya kulipuka kwa maambukizi mapya nchini humo .

Daktari Michael Ryan wa shirika hilo amesema kuwa sehemu za kulaza wagonjwa mahututi ( ICU) zimejaa wagonjwa licha ya mamlaka za nchi hiyo kudai kuwa idadi ya waliokutwa na janga hilo ni ndogo.

Mkuu huyo wa idara ya dharula ya WHO ameitaka China kuweka wazi hali halisi ya maambukizi hayo.

Hivi karibuni, hospitali katika mji mkuu wa Beijing na miji mingine zimeripotiwa kujaa wagonjwa.

Mwaka 2020, China imeweka utaratibu wa kufuatwa katika kampeni ya kuwa na maambukizi sefuri.

Hata hivyo, utaratibu huo umekuwa ukipingwa na kupelekea serikali kupunguza masharti hayo.

The post Hospitali China zaelemewa wagonjwa wa Covid -19 appeared first on KITENGE BLOG.



By Author

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post