JK AONGOZA KIKAO CHA BODI YA TAASISI YA KIMATAIFA INAYOSHUGHULIKIA ELIMI JIJINI PARIS, UFARANSA |Shamteeblog.

Rais Mstaafu Mheshimiwa Dkt. Jakaya Kikwete, ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya  Taasisi ya Kimataifa inayoshughulikia Masuala ya Elimu Duniani (Global Partnership for Education - GPE) akingoza Vikao vya Bodi ya Taasisi hiyo vinavyofanyika Jijini Paris,  nchini Ufaransa kuanzia tarehe 5 - 7 Disemba, 2022.  

Vikao hivyo ni vya kwanza vya ana kwa ana tangu dunia ilivyokumbwa na ugonjwa wa COVID-19 mwishoni mwa mwaka 2019.  Katika vikao hivyo, Taasisi ya GPE inapitia na kuazimia masuala mbalimbali yatakayolenga kuboresha mifumo ya elimu katika nchi zinazoendelea ikiwemo kuongeza idadi ya wanafunzi wanaopata elimu, wakiwemo watoto wa kike, na matumizi ya teknolojia katika utoaji wa elimu.






 


By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post