MACHINGA WILAYA YA KINONDONI WAIOMBA SERIKALI KUINGILIA KATI WANAOJIMILIKISHA MEZA ZAIDI YA MOJA KUFANYA BIASHARA |Shamteeblog.

Na Mwandishi wetu

WAFANYABIASHARA ndogo ndogo maarufu Machinga katika Wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam wameiomba Serikali kuingilia kati kitendo kinachofanywa na baadhi ya wafanyabiashara wakubwa kuhodhi eneo zaidi ya moja huku wao wakikosa eneo hata la kuweka meza kufanya biashara.

Wamedai wanalazimika kusubiri jioni ndio wapange biashara kwenye maeneo ambayo yamezuiliwa jambo ambalo limekuwa changamoto kubwa kwao na  hivyo wanaona njia pekee ya wao kuwa kupata maeneo ya biashara ni Serikali kuingilia kati.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa Machinga Wilaya ya Kinondoni Abdalah Mwakilimo amesema wanaishukuru Serikali kwa kuweka utaratibu mzuri wa maeneo ya kufanyia shughuli zao lakini changamoto kubwa ni baadhi ya watu wasio na huruma  kujimilikisha eneo kubwa.

"Wanachokifanya ni  kinyume na utaratibu na uongozi wa Sokoni ukiwafuata huwa wakaidi kutokana nyuma yao kuna baadhi ya maofisa wa idara ya biashara wanawakingia kifua kwasababu wanazozijua wao.Nimechaguliwa kuwa kiongozi kutetea Machinga Wilaya hii ya Kinondoni.

"Lakini  napitia wakati mgumu kwani  Machinga wenzangu wamekuwa wakilalamika kukosa maeneo ya biashara huku wakiona baadhi ya wenzao wanamiliki maeneo makubwa, hivyo  utakuta mtu mmoja ameweka biashara zake katika eneo moja meza  zaidi ya tisa akiwa ameyaandikisha majina ya watoto wake.

"Nikimfuata kumueleza najibiwa vibaya na kutishiwa .Naomba ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri tusaidiane kutatua changamoto hii," amesema Abdallah na kuongeza Serikali imetoa utaratibu wa Machinga kulingana na mitaji yao ikiamini kuwa atakuwa akifanya shughuli zake huku akitoka hatua moja kwenda nyingine.

Ameongeza hivyo  hadi kufikia kuwa mfanyabiashara mkubwa lakini watu wasio na huruma na ubinafsi ukiwa umewajaa mioyoni mwao hujimilikisha eneo kubwa huku wenzao wakikosa pa kuweka biashara zao hususani Makumbusho tatizo hili limekuwa sugu .

Amefafanua kwamba Machinga ni kundi linalotegemewa na  familia zao  ikiwemo watoto baba na mama hivyo wakikosa maeneo ya  kufanya shughuli zake Ili wajipatie kipato kwa ajili ya kukidhi mahitaji yao itasababisha   kundi kubwa lililopo nyuma yao  kuishi maisha magumu wakati mwingine watoto kukosa shule.

Hivyo  wanaiomba Serikali iangalie hao wanaohodhi maeneo makubwa na wenzao kukosa maeneo  wachukuliwe hatua stahiki.

Kwa upande wake Msemaji wa Machinga Wilaya ya Kinondoni Sharifu Hassan ameiomba Serikali kumpa nguvu Mwenyekiti kwani Masokoni humo amedai  kuna ufisadi mkubwa unaotendeka na watu wachache kujilikisha eneo kubwa ukiangalia hadhi yao siyo ya kuwa Machinga ila wanatumia mwamvuli huo kuwaimiza 

"Naishauri Serikali ni vyema maeneo ya biashara yanapogawiwa wawepo kwani kisheria Machinga anatakiwa amiliki meza moja akimiliki zaidi ya moja si Machinga tena atoke akapange fremu kwani machinga tupo wengi hivyo hata  Serikali ikiamua kufanya ukaguzi sisi hatuogopi tutawataja wote  wanaomiliki meza zaidi ya moja."

Wakati huo huo  Mfanyabiashara wa Makumbusho Sokoni Ally Dauda amesema hao  wanaomiliki maeneo makubwa hufanya udanganyifu wakati wa kuandikisha wengine huandika majina ya baba zao na watoto zao ambao hata umri wa miaka 18 hawajatimiza ambapo ni kinyume na utaratibu

Aidha Machinga  wa Wilaya hiyo   Wanashukuru Serikali ya Awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassani kuwatambua  kuwa wao ni kundi Maalumu hivyo wako chini ya Wizara Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto, Wanawake na Makundi Maalumu hivyo nao wanahitajika kupewa huduma na Serikali kitendo alichofanya Rais  na imesaidia taasisi za kifenda ikiwemo benki ya Maendeleo benki,NMB kuweza kuwaamini na kuwapatia mikopo Ili wafanye shughuli zao 

Pia wameiomba serikali  katika mwaka ujao wa 2023  Soko la Bunju litengenezewe miundombinu daladala,bajaji,pikipiki ziweze kuingia na kutoka Ili kusaidia soko hilo kuchangamka na Machinga wasiache meza zao na kuanza kutembeza bidhaa mitaani.

Mwenyekiti wa Wafanyabiashara ndogo ndogo 'Wamachinga' katika Wilaya ya Kinondoni Abdallah Mwakilimo akizungumza kuhusu changamoto ya machinga kukosa meza za kufanyika biashara.



By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post