Makabrasha ya mauaji ya JFK hadharani |Shamteeblog.

Ikulu ya Marekani imeruhusu kutolewa kwa makarani yenye kuelezea mauaji ya Rais wa zamani wa nchi hiyo John F Kennedy.

Rais huyo aliuawa kwa risasi iliyopigwa na mdunguaji ( Sniper) mwaka 1963 alipokuwa katika mji wa Dallas, Texas.

Sheria ya mwaka 1992 inaitaka serikali kutoa vielelezo vinavyoonyesha namna rais huyo alivyouawa kama sehemu ya historia.

Rais wa Marekani Joe Biden jana alitoa amri ya kiserikali ya kutolewa kwa vielelezo hivyo.

Hata hivyo, katika orodha ya karatasi 13, 173 , karatasi 515 zitaendelea kubaki katika hifadhi ya taifa ya nyaraka za nchi hiyo.

Shirika la uchunguzi la Marekani ( CIA) limesema kuwa nyaraka nyingine zinazohusiana na safari zake ikiwemo ile ya Mexico pia itatolewa.

Wakati wa utawala wa Rais Donald Trump, Rais huyo alitoa pia baadhi ya nyaraka hizo , lakini alificha baadhi kwa sababu za usalama.

Mwezi Oktoba mwaka 2021, Rais Biden pia alitoa nyaraka 1,500 huku nyingine akizuia.

The post Makabrasha ya mauaji ya JFK hadharani appeared first on KITENGE BLOG.



By Author

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post