Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV -Iringa
HALMASHAURI ya Manispaa ya Iringa imeamua kuchukua hatua dhidi ya kukabiliana na vitendo vya kikatilii ambavyo vinaendelea ndani ya Mkoa huo ambavyo vinachochewa na waganga wa kienyeji.
Hayo yamezungumzwa na Meya wa Manispaa ya Iring Ibrahim Gwada wakati anazungumza na Michuzi TV ambapo amefafanua ili kuondoa changamoto hiyo moja ya hatua waliyoichukua ni kukutana na viongozi wa dini zote ambao wao wamedai waganga wa kienyeji ndio chanzo kikubwa.
"Kwa mujibu wa viongozi wa dini ndani ya Manispaa yetu tulipokutana wamedai baadhi ya waganga wa jadi wamekua wakichangia kwa kiasi kikubwa ukatili wa kijinsia hasa ulawiti kwa watoto kutokana na dhana na imani potofu wanazozijenga kwa wananchi kwa masharti wanayowapa ikiwa ni pamoja na mambo ambayo yanasababisha ukatili katika jamii kwa dhana ya kufanikiwa kimaisha."
Aidha amesema amefanya jitihada za kukutana na waganga hao wa jadi ili kuzungumza namna ya kutatua changamoto hiyo ambapo kwa upande wao baadhi ya waganga wamekiri kuwapo kwa baadhi yao kukosa uadilifu.
"Baadhi ya waganga wamekiri kuwa baadhi yao waamekua sio waadirifu na kuwadanganya wananchi kufanya ukatiri hasa urawiti kwa watoto wadogo ni njia ya kujipatia mafanikio kimaisha."
Ameongeza kuwa kupitia kikao hicho baina yake na waganga wa jadi wameweka mikakati ya udhibiti waganga wasiofata maadili ambao pia wamekua wakichangia kuwapo kwa tatizo hilo.
By Mpekuzi
Post a Comment