Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu barani Afrika ( CAF) Patrice Motsepe amesema kuwa moja wapo ya nchi za Afrika itafika fainali katika fainali zijazo za kombe la Dunia.
Motsepe, raia wa Afrika ya Kusini amesema kwa namna ambavyo timu za Afrika zimepambana katika michuano ya kombe la dunia iliyomaliza nchini Qatar, moja ya timu kutoka bara hilo itafika fainali katika michuano ya mwaka 2026.
Morocco imefanikiwa kufika hatua ya Nusu Fainali ya michuano iliyomalizika nchini Qatar.
Imekuwa ni timu ya kwanza barani Afrika kufanikiwa kufika hatua hiyo.
Hii ni baada ya timu nyingi za Afrika kuishia hatua ya robo fainali tu katika michuano ya nyuma.
” Nina hakika moja ya timu kutoka Afrika itafika fainali michuano ijayo,” amesema.
” Ni wakati wa kujivunia kwa soka la Afrika,”
“Matarajio makubwa ni kuona bara la Afrika likishinda taji la kombe la Dunia,” amesema.
” Lakini pia nina amini uwezo wa Morocco na mafanikio ya timu nyingine za Afrika utaongeza chachu ya ushindani katika soka la Afrika,” amesema.
The post Motsepe aitabiria makubwa Afrika kombe lijalo la Dunia appeared first on KITENGE BLOG.
By Author
Post a Comment