Rais Mwinyi awasili Dodoma |Shamteeblog.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi-CCM, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi, akiambatana na mkewe Mama Mariam Mwinyi, amewasili Dodoma jioni hii tayari kuhudhuria vikao vya kikatiba vya Chama cha Mapinduzi na Mkutano Mkuu wa CCM Taifa utaofanyika tarehe 07/12 na tarehe 08/12.

Katika uwanja wa ndege wa Dodoma, Dk. Mwinyi alilakiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule pamoja na viongozi wengine wa Chama na serikali wa mkoa wa Dodoma.

The post Rais Mwinyi awasili Dodoma appeared first on KITENGE BLOG.



By Author

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post