SENEGAL WASHINDWA KUPANDA MLIMA MREFU |Shamteeblog.

 



Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

Timu ya taifa ya Senegal imetupwa nje ya Michuano ya Kombe la Dunia 2022 baada ya kufungwa mabao 3-0 na timu ya taifa ya Uingereza katika mchezo wa hatua ya 16 Bora ya Michuano hiyo kwenye mchezo uliopigwa kwenye dimba la Al Bayt.

Simba wa Teranga walianza kupoteza matumaini ya kusonga mbele kwenye Michuano hiyo baada ya kufungwa bao la kwanza na Kiungo Jordan Henderson kwenye dakika 38’, bao la pili lilifungwa na Mshambuliaji Harry Kane dakika ya 45+2’ huku Mshambuliaji Bukayo Saka akashindilia msumari wa tatu dakika ya 57’.

Ni dhahiri Uingereza wamefuzu hatua ya Robo Fainali ya Michuano hiyo ya Kombe la Dunia inayoendelea nchini Qatar na watakutana na Bingwa mtetezi wa Michuano hiyo, timu ya taifa ya Ufaransa ambao wamefuzu hatua hiyo baada ya kuwatupa nje Poland.

Senegal wanarudi nyumbani Dakar baada ya safari yao ya kulisaka taji la dunia kuishia hapo hatua ya 16 Bora, timu pekee iliyobaki kutoka bara la Afrika ni Morocco ambao watacheza mchezo wao wa hatua hiyo ya 16 Bora dhidi ya Hispania, Desemba 6 mwaka huu. 

Timu za bara la Afrika zilizorudi nyumbani ni Cameroon, Tunisia, Ghana ambao wametupwa nje ya Michuano hiyo katika hatua ya makundi wakati Senegal na Morocco ni timu pekee zilizofanikiwa kufuzu hatua ya 16 Bora na sasa imebaki Morocco pekee.




By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post