Na Mwandishi Wetu.
Spika mstaafu wa Bungee la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anna Makinda Leo ameongoza mahafali ya 20 ya chuo Cha Herbert Kairuki kilichopo Mikocheni Jiji Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa mahafali hayo Mkuu wa chuo hicho Spika Mstaafu Anna Makinda Amesema chuo hicho kimekuwa mstari wa mbele katika kutoa taaluma ambayo itawasaidia wa Tanzania.
“Katika mahafali yetu ya kwanza mwaka 2003 wahitimu walikuwa 63 wakiwemo madaktari wanne na wengine wakiwa wauguzi lakini leo hii katika mahafali haya ya 20 tuna wahitimu 294 na idadi hii inafkisha jumla ya wahitimu 3,186 miongoni mwao wakiwemo madaktari wa binadamu 1,560,” alisema
Alisema Shirika la Afya Duniani (WHO), linapendekeza uwiano wa daktari mmoja kwa wagonjwa 8,000 na kwamba uwiano huo kwa hapa Tanzania bado hauridhishi kwani daktari mmoja anakadiriwa kuhudumia wagonjwa 20,000 kwa mwaka.
“Ingawa mahitaji bado ni makubwa tunamshukuru Mungu kwamba tumeweza kuendelea kutoa mchango wetu kwa taifa katika kupunguza uhaba wa rasilimali watu katika sekta ya afya mwaka hadi mwaka kwa miaka 25 mfululizo,” alisema
Mkuu wa chuo hicho, Anne Makinda alisema chuo hicho tangu kuanzishwa kwake kimekuwa kikitoa wahitimu bora wenye weledi wa hali ya juu ambao wanafanyakazi kwenye maeneo mbalimbali ndani na n je ya nchi.
“Juzi tulikuwa na kusanyiko la kitaaluma walikuja waliowahi kusoma HKMU kwa kweli ukiwasiliza wanavyowasilisha mada zao wanavyojiamini unapata uhakika kabisa kwamba hapa ni sehemu sahihi ya kufundisha watumishi wa kada ya afya,” alisema
Naye Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Yohana Mashalla, aliomba serikali ipunguze gharama za vifaa vya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano TEHAMA ili wanafunzi wengi zaidi waweze kusoma kwa njia ya mtandao.
Profesa Mashalla aliiomba serikali kuvipa ruzuku kwa vyuo viuu binafsi ili vijiandae kwa kuwekeza kwenye ujenzi wa miundombinu, kusomesha wahadhiri na ununuzi wa vifaa vya kufundishia, maabara na maktaba ili kukidhi mahitaji ya kuongezeka kwa mahitaji ya elimu ya juu nchini.
Aidha, alisema katika kukabiliana na changamoto ya uhaba wa wahadhiri, HKMU imeendelea kufadhili masomo ya wahadhiri katika ngazi ya uzamili na uzamivu ndani na nje ya nchi.
Alisema kwa sasa jumla ya wahadhiri 14 wako masomoni, kati yao saba masomo ya uzamivu na wengine saba masomo kwa ngazi ya uzamili..jpeg)
.jpeg)
Mwenyekiti wa Baraza la chuo cha HKMU John Ulanga akizungumza kwenye mahafali ambayo yamefanyika leo Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki (HKMU), Anne Makinda akimtunuku Shahada ya udaktari bingwa mmoja wa wahitimu wa udaktari bingwa kwenye mahafali ya 20 ya chuo hicho yaliyofanyika leo chuoni hapo Mikocheni jijini Dar es Salaam..jpeg)
.jpeg)
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki (HKMU), Anne Makinda akiongoza msafara kutoka kwenye mahafali ya 20 ya chuo hicho yaliyofanyika leo chuoni hapo Mikocheni jijini Dar es Salaam, kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mtandao wa Elimu ya Afya Kairuki (KHEN), Mama Kokushubira Kairuki.

By Mpekuzi
Post a Comment