Uingereza yaifungasha virago Senegal |Shamteeblog.

Timu ya Taifa ya Uingereza imefuzu hatua ya robo fainali ya kombe la Dunia 2022 baada ya kuwacharaza Simba wa Teranga Senegal bao 3-0 katika mchezo wa hatua ya 16 bora uliopita katika dimba la Al Bayt, Qatar.

Magoli ya Uingereza yamefungwa na Jordan Hendeson, Harry Kane na Bukayo Saka.

Kufungwa huko kwa mabingwa hao wa Afrika kumehitimisha safari yao kurudi nyumbani huku Uingereza ikisonga mbele hatua ya Robo Fainali.

England sasa itakipiga dhidi ya mabingwa watetezi Ufaransa kwenye hatua ya robo fainali itakayopigwa Jumamosi, Disemba 10, 2022 majira ya saa 4:00 usiku.

Ufaransa nao wamefanikiwa kutinga Robo Fainali baada ya kuwafunga Poland 3-1.

The post Uingereza yaifungasha virago Senegal appeared first on KITENGE BLOG.



By Author

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post