TFS WAPANDA MITI YA MIKOKO WAKIADHIMISHA SHEREHE ZA MIAKA 59 YA MAPINDUZI ZANZIBAR |Shamteeblog.

Na Said Mwishehe, Michuzi TV

WAKALA wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) wameadhimisha sherehe za miaka 59 ya
Mapinduzi Matukufu ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kupanda miti ya mikoko 350 katika
eneo la Kunduchi Mtongani wilayani kinondoni mkoani Dar es Salaam.

Akizungumza leo Januari 12,2023 wakati wa upandaji wa miti hiyo ya mikoko, Katibu Tawala
wa Halmashauri ya Wilaya ya kinondoni Stella Msofe amesema mikoko hiyo itatunzwa kama
ambavyo wamekuwa wakitunza mikoko ndani ya wilaya hiyo pamoja na mazingira kwa ujumla.

Aidha amesema halmashauri hiyo itahakikisha inalinda maeneo yote yenye uhifadhi wa mazingira
sambamba na kuondoa watu wote ambao wamevamia maeneo ambayo yamekuwa na mikoko hasa ya mwambao wa bahari ya Hindi katika halmashauri ya wilaya ya kinondoni.

Katibu Tawala huyo aliyekuwa amwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Godwin Gondwe,
amesema katika kulinda maeneo hayo hawatasita kubomoa majengo yaliyojengwa kwenye maeneo
yenye hifadhi ya mikoko.

Amesema Halmashauri ya Wilaya ya Kinondoni haitasita kuchukua hatua kwa watu wote
wanaojihusisha na uharibifu wa mazingira ya fukwe za bahari pamoja na mikoko hiyo.

;Nitoe rai kwa wananchi wa Kunduchi na maeneo mengine ya Kinondoni hasa walio karibu na mwambao kutojihusisha na uharibifu wa mazingira unaoathiri mikoko na naendeleo ya mazao ya bahari.Serikali inahakikisha mazingira yote ya bahari yanalindwa.”


Kwa upande wake Kamanda wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) Kanda ya Mashariki inayosimamia mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Morogoro, Mathew Ntilicha amesema wameadhimisha sherehe hizo za mapinduzi kwa kupanda miti ya mikoko.

“Kama nchi inapitia mabadiliko ya tabianchi hivyo mikoko ni misitu muhimu katika kukabiliana na
hali hiyo pia ina uwezo wa kunyonya hewa chafu mara 10 ya misitu ya asili.”

Wakati huo huo Mhifadhi Mkuu wa TFS Frank Sima amesema nchini Tanzania kuna Wilaya 14 zenye mikoko na Wilaya ya Kinondoni ni mingoni mwao huku akitumia nafasi hiyo kuelezea hatua mbalimbali zinazochukuliwa na TFS kwa kushirikiana na wadau wengine kupanda mikoko na miti mingine ili kurejesha misitu.


Aidha amesema upandaji huo wa mikoko ni kuunga mkono jitihada za Rais Samia Suluhu
Hassan za uhifadhi wa mazingira.

Kwa upande wake Mhifadhi Mkuu Wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam Dotto Ndumbikwa ameongeza kwamba wamepanda mikoko hiyo kwa kuwa Kunduchi imeathirika baada ya mmoja ya watu ambaye anadaiwa kuwa na tatizo la akili kukata mikoko iliyokuwepo eneo hilo.
Katibu Tawala wa Halmashauri ya Wilaya ya kinondoni mkoani Dar es Salaam Stella Msofe(wakwanza kulia) akiwa na makamishna wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) Kanda yaMashariki wakipanda miti ya mikoko katika eneo la Kunduchi Tuangoma leo Januari 12,2023 ikiwani sehemu ya Maadhimisho ya sherehe za miaka ya 59 ya Mapinduzi ya Zanzibar.





Matukio mbalimbali kwenye picha wakati wa kupanda miti ya mikoko eneo la Kunduchi Tuangoma wilayani Kinondoni mkoani Dar es Salaam.


By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post