DC Monduli: VETA ni mkombozi kwa vijana kupata elimu ya ufundi na ujuzi |Shamteeblog.

*Jamii wafugaji wakubali kusoma katika Chuo cha VETA Monduli.

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV Monduli
MKUU wa Wilaya ya Monduli Suleiman Mwenda amesema kuwa ujenzi wa vyuo vya ni ukombozi kwa vijana kupata ujuzi wa kuweza kuajiriwa au kujiajiri kutokana na dhamira ya serikali kuwa katika uwekezaji wa viwanda.

Mwenda aliysema hayo wakati alipotembelea Ujenzi wa Chuo cha VETA Monduli , amesema kuwa ujenzi wa vyuo vya VETA ni mkombozi kwa vijana kutokana kila mwaka kwa wanaobaki kuendelea na ngazi ya Elimu inayofuata na kubaki bila kuwa kitu chochote lakini VETA ndio mkombozi wa vijana.

Amesema kwa Takwimu zilizopo wanafunzi wa darasa la kwanza wakiandikishwa watapofika darasa la Saba wengine wanabaki wengine wanaendelea kidato cha kwanza hadi kidato cha nne ambapo wengine wanaendelea na kidato cha Tano na Sita na hapo wengine wanaenda Chuo Kikuu na kubaki kundi lingine haliendi Chuo kikuu ambapo makundi yote yanatakiwa kupata ujuzi na baadae kujiajiri au kuajiriwa.

Mwenda amesema ujenzi wa Chuo cha VETA iko sehemu ya Ilani hivyo limetekelezwa kwa vitendo katika kuhakikisha wananchi wanapata elimu ya ufundi ambapo mwisho wa siku watatengeneza kipato cha kuendesha maisha na kupata na kukua kwa uchumi.

Aidha amesema kuwa jamii ya Monduli ni wafugaji lakini wameitikia kupata elimu kwa kuamini ndio mafanikio ya kupata mafundi wa aina mbalimbali.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Makuyuni Lucas Mollel amesema kuwa wafugaji wa kabila la wamasai hawana cha kushika kwa sasa kwani Ng'ombe wanakufa na hata hawazaliani ambapo kwa sasa ni kusoma na chuo kimejengwa.


Diwani wa Kata ya Makuyuni wilayani Monduli Elias Pusindawa amesema kuwa Chuo cha VETA kifunguliwe ili vijana waanze kusoma ili malengo ya Serikali ya awamu ya Sita ya Dk.Samia Hassan Suluhu yatimie ya kuhakikisha wana Monduli wanapata elimu.


Amesema kuwa majengo ya 17 yaliyojengwa katika Chuo ni ya kiwango na wananchi wetu wameshiki kutokana mafumo wa Force Account kwa mafundi wa eneo husika la mradi.


Kaimu Mkuu wa Chuo cha VETA Mkoa wa Manyara Gulnat Nzowa amesema ujenzi wa Chuo hicho umefikia asilimia 97 ambapo wanatarajia mwezi Aprili waanze masomo.


Amesema kuwa Chuo cha VETA cha Mkoa wa Manyara ndio kimejenga chuo cha VETA Monduli ambapo majengo yote yako imara na kutaka wananchi wayatunze majengo hayo kwa vizazi na vizazi.
Mkuu wa Wilaya ya Monduli mkoani Arusha Suleiman Mwenda akipata maelezo kwa Mwalimu wa Ujenzi wa Chuo cha VETA Mkoa wa Manyara Isaac Malema wakati wa alipootembelea kuangalia ujenzi wa Chuo cha Monduli kinachojengwa na Chuo cha Manyara.
Mkuu wa Wilaya ya Monduli mkoani Arusha Suleiman Mwenda akizungumza na waandishi wa Habari kwenye mradi wa Ujenzi wa Chuo cha VETA Monduli kilichojengwa Makuyuni.
Jengo la Utawala la Chuo cha VETA Monduli
Mkuu wa Wilaya Monduli mkoani Arusha Suleiman Mwenda akiwa na baadhi ya watendaji wa VETA Mkoa wa Manyara pamoja na viongozi wa Serikali wa wilaya hiyo.


By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post