Kesi ya KKKT Njombe yaahirishwa hadi February 17 |Shamteeblog.


Njombe

Mahakama ya Hakimu mkazi Njombe imeahirisha kesi No 2,2022 ya madai ya fidia ya shilingi Mil 100 iliyofunguliwa na msimamizi wa mirathi wa marehemu Kaselida Mlowe dhidi ya kanisa la kiinjili la kirutheli Tanzania Dayosisi ya kusini mpaka February 17 kutokana na hakimu mfawidhi wa Mahakakama hiyo kuwa safarini.

Mahakama imeahirisha kesi hiyo ya madai iliyofunguliwa na msimamizi wa mirathi baada ya mlalamikaji kushinda trafic kesi no 6 ,2021 iliyotokea eneo la Kibena katika mlima Ichunilo septemba 25,2020 iliyohusisha gari aina ya Hiace yenye nambari za usajiri T298-DNE na gari aina ya Mercedez Benz Truck yenye nambari za usajiri T210-AHU mali ya kanisa ambayo ilipelekea kifo cha Kaselida Karo Mlowe ambaye aliacha watoto wadogo watatu.

Katika kesi ya kwanza ya ajali ya barabarani iliyosimamiwa na hakimu wa wilaya ya Njombe Matrida Kayobo iliyosababisha majeruhi na kupelekea kifo cha Kaselida Mlowe,Mahakama ilimkuta na hatia dereva aliyekuwa akiendesha gari hiyo ya kanisa hatua iliyompa mamlaka mlalamikaji ya kufungua kesi ya fidia dhidi ya mlalamikiwa ili kusaidia watoto walioachwa na Marehemu.

Akizungumzia hatua hiyo wakili wa upande wa mlalamikaji Gervas Semgamo kwa niaba ya mawikili Emmanuel Chengula na Frank Ngafumika amesema baada ya hatua mbalimbali ya matakwa ya keshiria juu ya shauri hilo kesi hiyo ya madai ilitarajiwa kuanza kusikilizwa tarehe 3 lakini imeweza kuahirishwa mpaka tarehe 17.




By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post