Kilichomkuta Sheikh Alhad Akihangaika Kuvunja Ndoa ya Dr Mwaka |Shamteeblog.


Baraza la Ulamaa katika kikao chake kilichoketi jijini Dar es salaam, limetengua uteuzi wa Sheikh Alhad Mussa Salum, kama Sheikh wa mkoa wa Dar es salaam kuanzia 02 February 2023. Baraza hilo limemteua Sheikh Walid Alhad Omary kuwa Kaimu Sheikh wa mkoa wa Dar kuziba nafasi ya Sheikh Alhad.

Itakumbukwa wiki jana Sheikh Alhad kwa kushirikiana na baraza la masheikh wa mkoa wa Dar, alivunja ndoa ya Juma Mwaka na mkewe Queen, lakini kesho yake Baraza la Ulamaa lilibatilisha uamuzi huo na kufuta talaka hiyo. Hata hivyo Sheikh

Alhad aliemdelea kusisitiza kuwa talaka hiyo ni halali na ndoa hiyo imevunjwa.

Kesho yake Baraza la habari la habari la BAKWATA lilitoa tamko la kupinga maamuzi ya Baraza la Ulamaa na kusema linasimama na Sheikh Alhad kuvunja mdoa hiyo.

Baraza la Ulamaa ambalo ndio chombo kikuu cha maamuzi ndani ya BAKWATA lilitoa onyo kwa Masheikh hao pamoja na Sheikh Alhad, na kuwataka waombe radhi. Hata hivyo hawakuomba radhi, mpaka juzi Sheikh Alhad alipopigwa na kitu kizito.!



from Author

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post