Koka amuunga mkono Rais Samia kukiimarisha chama kwa vitendo |Shamteeblog.


Na Victor Masangu,Kibaha

Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka katika kutekeleza ilani ya chama kwa vitendo ameamua kukabidhi kadi zipatazo 400 katika matawi yapatayo nane yaliyopo katika kata ya mail moja lengo ikiwa ni juhudi za kuongeza idadi ya wanachama zaidi.

Koka amekabidhi kadi hizo wakati wa ziara ya kamati ya siasa ya chama cha mapinduzi kibaha mjini ambapo amesema nia na madhumuni ni kukiimarisha chama zaidi ili kiweze kufanya vizuri katika chaguzi mbali mbali.

Mbunge huyo alisema kuwa lengo lake kubwa ni kuhakikisha anawatumikia wananchi kwa vitendo hivyo moja ya kukiimarisha chama ni kuongeza idadi ya wanachama ambao wataweza kuleta mabadiliko katika kukiimarisha chama cha mapinduzi.

Alisema kuwa juhudi ambazo zinafanywa na Rais wa awamu ya sita Mama Samia Suluhu Hassan katikakukiimarisha chama zinapaswa kuungwa mkono ndio maana akaamua kukabidhi kadi hizo kwa maslahi ya wanachama na chama chenyewe.

Kadhalika koka katika ziara hiyo Mbunge huyo alikabidhi bendera kwa mabalozi wa kata ya maili moja na kuwahimiza mabalozi wa matawi kuwahimiza wanachama wengine kujiunga na chama hicho.

Pia alisema ataendelea kushitikiana bega kwa bega na wananchi wote wa Jimbo lake la Kibaha mjini ili kusikikiza changamoto zao mbali mbali na kuweza kuzitafutia ufumbuzi katika nyanja mbali mbali.

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) katika Wilaya ya Kibaha mjini Fatma Nyamka amewataka viongozi wa matawi na mashina kuweka mikakati ya kuongeza idadi ya wanachama wengine wapya.

Aidha Nyamka aliwataka wanachama kwa sasa kubadilika na kuachana kabisa na kuunda makundi kwani uchaguzi umeshamalizika na badala yake waungane kwa pamoja katika kukijenga chama.

Sambamba na hilo Mwenyekiti huyo aliwashukuru wanachama kwa kuamua kumchagua katika nafasi ya uenyekiti na kuahidi kuwapa ushirikiano wa kutosha katika kutekeleza ilani ya chama kwa vitendo.

Kamati ya siasa ya chama Cha mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kibaha mji imefanya ziara katika kata ya mail moja ambapo imepata fursa ya kuzungumza na wanachama pamoja na kuwatembelea viongozi mbali mbali wa mashina na matawi.




By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post