Malkia wa mipasho ya taarab Khadija Kopa amefunguka kuhusu maisha yake tangu kufiwa na mume wake marehemu babake Zuchu mwaka 2013 na kile anachokitazamia katika maisha ya siku za baadae.
Kopa anasema kuwa tangu mumewe kufa, hajawahi pendana na mwanamume mwingine huku sasa akitangaza mipango ya kutaka kurudi kwenye kidimbwi cha mapenzi na mwanamume aliyekomaa.
Alisema kuwa anatazamia kumpata mwanamume komavu, ikiwezekana miaka 50 kwenda mbele ambaye anajiweza vizuri pande zote kuanzia mfuko hadi masuala ya faraghani, na awe mcha Mungu.
“Mimi jimbo liko wazi, tangu marehemu mume wangu afariki niko peke yangu. Mjumbe akija lazima awe na umri mkubwa, kuanzia miaka 50 kwenda juu, awe anajiweza anaweza kunitunza mimi mkewe sio yakhe sababu niko pale, akija tutasaidiana, shida zangu azijue, awe anamuogopa MUNGU awe mtu wa dini,” Mamake Zuchu alisema.
Malkia huyo wa midundo ya Taarab alisisitiza kuwa hana nia ya kulea kiben10 kwani nia yake ya kuzama mjini Dar es Salaam ni kutafuta pesa na kujitunza, na akipata mwanamume wa kumtunza bora awe Zaidi ya miaka 50 itakuwa Zaidi ya Baraka kwa maisha yake.
“Nimekuja Dar kutafuta maisha, na nimekuja kikazi kwa hiyo sauti yangu lazima niitunze hii ndo hazina yangu.”
Alifichua kwamba hatumii pombe wala sigara wala kitu chochote cha kulevya, na ndio sababu kuu amekuwa kwenye kilele cha muziki wa taarab tangu miaka ya 90.
By Moses Sagwe
from Author
Post a Comment