Rais wa Moldovia aishutumu Urusi kutaka kuipindua serikali yake |Shamteeblog.

Rais wa Moldova ameishutumu serikali ya Urusi kwa kutaka kuipindua serikali yake.

Maia Sandu amedai kuwa Urusi inawatumia watu waliopo nchini humo kufanya mipango hiyo.

Jana Ijumaa Rais huyo amefanya mabadiliko ya Waziri Mkuu na kumteua Dorin Receau ambaye ana mlengwa tofauti.

Rais huyo amesema mpango uliopangwa wa kuiangusha serikali yake ni kupitia maandamano yenye lengo la kupinga katiba.

Vita ya Urusi na Ukraine imeiweka pabaya Moldovia, moja ya nchi masikini sana katika bara la Ulaya.

Wiki iliyopita, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema kwa mujibu wa taarifa za kishushushu alizonazo, Urusii ina mpango wa kuipindua serikali ya Moldovia.

The post Rais wa Moldovia aishutumu Urusi kutaka kuipindua serikali yake appeared first on KITENGE BLOG.



By Author

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post