Thamani Ya Staa Wa Manchester City Erling Haaland Kwa Sasa Ni Euro Bilioni 1 |Shamteeblog.

 


UMESIKIA hiyo, thamani ya staa wa Manchester City, Erling Haaland kwa sasa ni euro bilioni 1.


Haya yameelezwa na wakala wa staa huyo, Rafaela Primenta ambaye anamsimamia Haaland na mastaa wengine akiwemo Paul Pogba, Marco Verratti, Gianluigi Donnarumma, Matthijs de Ligt.


Staa huyo ndani ya Manchester City kwenye Premier msimu huu amefanikiwa kufunga mabao 26, huku Ligi ya Mabingwa Ulaya akifunga mabao matano katika mechi nne.


Pimenta alisema: “Erling Haaland kwa sasa thamani yake ni euro bilioni 1 na kwenye hili nipo siriazi, hii ndiyo thamani yake.


“Kuhusu hatma ya Marco Verratti, kwa kweli ni ngumu kuona anakwenda katika klabu nyingine, anaipenda Paris Saint-Germain na anataka kuwa pale.”


Ikumbukwe kuwa, licha ya Haaland kutua ndani ya Manchester City msimu huu, lakini  bado staa huyo anawindwa na klabu kubwa kama Real Madrid.



from Author

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post