Afisa Habari wa Klabu ya Yanga SC, Ali Kamwe amesema kuwa amezungumza na Mshambuliaji wa Timu hiyo Fiston Mayele na kumwambia kuwa inabidi aipe Yanga Milioni 10 kwa kufunga magoli mawili katika mchezo wao wa Kimataifa wa Shirikisho Afrika dhidi ya TP Mazembe ya Congo siku ya Jumapili.
Akiwa kwenye Kipindi cha Number Ten cha TVE ameyasema hayo kutokana na ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kuwa atatoa Milioni Tano kwa kila Goli litakalofungwa na Simba na Yanga katika Michuano hiyo ya Kitaifa.
from Author
Post a Comment