Rihanna hakulipwa chochote kutumbuiza kwenye Halftime ya Super Bowl 2023, ni utamaduni uliozoeleka kwa NFL kutomlipa msanii pesa yoyote. Msemaji wa NFL Joanna Hunter aliwahi kukaririwa mwaka 2016 akiliambia Jarida la Forbes kwamba wao hawamlipi msanii bali wanamsaidia gharama za ziada kama za uandaaji (production costs) na matumizi mengine.
Mwaka 2021, Jarida la Forbes lilikadiria kwamba The Weeknd alitumia takribani ($20 million) zaidi ya TSh. Bilioni 46 kuandaa onesho lake kwenye fainali hizo za Super Bowl.
Licha ya Riri kutolipwa kutumbuiza kwenye onesho lake la kwanza ndani ya kipindi cha miaka 7, namba za mauzo ya nyimbo zake zimepaa sio kawaida kwenye mtandao wa Spotify. Streams za muziki wake zimepanda kwa asilimia 640 kwenye Spotify Marekani.
Wimbo wa “B*tch Better Have My Money” streams zake zimepanda kwa 2,600% huku “Diamonds” ikiongezeka kwa 1,400% na nyingine kama “Rude Boy" na “We Found Love”
from Author
Post a Comment