Naibu waziri Ofisi ya waziri mkuu kazi, vijana, Ajira na wenye ulemavu ambaye pia ni mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Katambi ameipongeza Jumuiya ya wazazi wa Chama Cha Mapinduzi Shinyanga Mjini kwa kuanzisha mradi wa utengenezaji wa tofali kwa ajili ya kujiendeleza kiuchumi.
Katambi ametoa pongezi hizo leo Desemba 16, 2023 wakati alipotembelea mradi huo uliopo kata ya Kambarage manispaa ya Shinyanga.
Awali akizungumza wakati wa kikao cha mwaka cha baraza la Jumuiya ya wazazi ya Chama Cha Mapinduzi Shinyanga Mjini Mwenyekiti wa baraza hilo Fue Mlindoko amesema wamejipanga kusimamia kikamilifu utekelezaji wa miradi hiyo inayoenda kuanzishwa ili iweze kunufaisha Jumuiya ya wazazi ya Chama Cha Mapinduzi Shinyanga Mjini.
"Sisi kama Jumuiya ya wazazi tumezamilia kuanzisha miradi ambayo kujialisha kisiasa na kiuchumi, kupitia kamati ya utekelezaji tumejipanga kufanya kazi kubwa ya kujenga Jumuiya imara miongoni mwa miradi tuliyoanzisha tumeanzisha kiwanda kidogo cha utengenezaji wa tofali za ujenzi kupitia kamati ya utekelezaji tutaendelea kusimama imara na kufikia malengo tuliyojiwekea", amesema Fue Mlindoko.
Katibu wa Jumuiya ya wazazi wa Chama Cha Mapinduzi Shinyanga Mjini Doris Kibabi amesema mradi huo umegharimu kiasi cha Shilingi milioni 9,300,000 ikihusisha ununuzi wa mashine mbili za utengenezaji wa tofali, kalo la kuhifadhia maji, umeme, mafundi pamoja na vifaa vingine.
Kwa upande wake Naibu waziri Ofisi ya waziri mkuu kazi, vijana, Ajira na wenye ulemavu ambaye pia ni mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Katambi ameipongeza Jumuiya ya wazazi ya Chama Cha Mapinduzi Shinyanga Mjini kwa kuanzisha mradi wa utengenezaji wa tofali na kuahidi kama mbunge wa jimbo hilo kutafuta masoko kupitia miradi inayotekelezwa maeneo mbalimbali ndani ya manispaa ya Shinyanga.
"Miradi hii inayoanzishwa ni ya kila mmoja wetu kwenye Jumuiya ya wazazi wa Chama Cha Mapinduzi Shinyanga Mjini na msimamizi wa miradi inayotekelezwa na Jumuiya hii, tunao viongozi wazuri wa wa usimamizi wa miradi yetu, nitoe ahadi kwenu kutafuta masoko ya ununuzi wa tofali kutoka kwenye kiwanda hiki kupitia miradi ya ujenzi inayotarajia kuanza utekelezaji ikiwemo ujenzi wa stendi kuu ya Shinyanga, Shule pamoja na soko kubwa la kisasa,"
"Niipongeze sana Jumuiya ya wazazi Shinyanga Mjini kwa kuanzisha mradi huu na kuendelea kujiimarisha kisiasa na kiuchumi, lakini pia kupitia mradi huu vijana wengi watanufaika kwa kupata ajira na wengine kufanya biashara jirani na eneo hilo", amesema Mhe. Katambi.
"Kama mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi tumeendelea kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa barabara, madaraja, shule na masoko, na ifikapo 2025 tutakuwa tumekamilisha yale yote niliyoahidi ndani ya manispaa ya Shinyanga, tuendelee kumuombea Rais wetu Mhe. Samia Suluhu Hassan kupitia serikali ya awamu ya sita kwa kuendelea kutoa fedha za ujenzi wa miradi mikubwa ndani ya mkoa wa Shinyanga", ameongeza Mhe. Katambi.
Aidha katika kikao cha baraza la Jumuiya ya wazazi wa Chama Cha Mapinduzi Shinyanga Mjini kilichoketi leo kimehusisha ugawaji wa vyeti vya pongezi kwa waliofanikisha ujenzi wa mradi huo pamoja na kuunda kamati ndogo ndogo zitakazosaidia jumuiya hiyo katika utendaji kazi.
By Mpekuzi
Post a Comment