UTEUZI: Rais Samia Atengua, Ateua na Kuhamisha |Shamteeblog.

 

UTEUZI: Rais Samia Atengua, Ateua na Kuhamisha

Rais Samia Suluhu Hassan jana Jumatatu Desemba 18, 2023 amefanya uteuzi, utenguzi na uhamisho wa vituo vya kazi vya watumishi mbalimbali wa Serikali wakiwamo wakurugenzi wa halmashauri, balozi na mwenyekiti wa bodi.


Katika taarifa kwa umma iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu imesema, Rais Samia amemteua Balozi Meja Jenerali Paul Simuli kuiwakilisha Tanzania nchini Uganda.


Aidha, amemteua Selwa Hamid kuwa Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya Igunga akichukua nafasi ya Francis Msabila aliyesimamishwa kazi.


“Amemteua Mariamu Chaurembo kuwa Mkurugenzi Mtendaji Halmshauri ya Mji Tunduma akichukua nafasi ya Lena Nkya ambaye uteuzi wake umetenguliwa.


“Amemteua Fabian Said kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Momba, akichukua nafasi ya Butamo Nuru ambaye uteuzi wake umetenguliwa,” imesema taarifa hiyo.


Aidha, amemuhamisha kituo cha kazi Dk Peter Nyanja aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Muleba na kwenda Halmashauri ya Wanging’ombe, Dk Nyanja anachukua nafasi ya Maryamu Muhaji ambaye aliteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Manyara.


Pia, Rais Samia amemteua Dk Khamis Mwinyimvua kuwa Mwenyekiti ya Bodi ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania, Dk Mwinyimvua ambaye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) anachukua nafasi ya Profesa Longinus Rutasitara aliyemaliza muda wake.



from Author

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post