SERIKALI imesema wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza katika Shule za Serikali kutwa na bweni hakuna atakayekosa nafasi kwani Serikali imetenga Sh bilioni 140.5 kwaajili ya ujenzi wa madarasa mapya sambamba na ukarabati wa madarasa yaliyopo kuelekea muhula mpya wa masomo utakaoanza Januari 08, 2024.
Hayo yametanabahishwa na Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mohamed Mchengerwa katika taarifa yake kwa umma katika mkutano wake na viongozi wa ngazi za Mikoa na Wilaya, uliofanyika ndani ya ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.
“Uchaguzi ulihusisha wanafunzi 1,092,984 wakiwemo wasichana 507,933 na wavulana 585, 051 ambao walifaulu mtihani wa kuhitimu Elimu ya Msingi mwaka 2023.” amesema waziri huyo.
Amesema vigezo vilivyotumika kuchagua wanafunzi hao ni kwa kuangalia waliopata alama za ufaulu kati ya 121 hadi 300, miongoni mwao hakuna asiyepangiwa shule.
“Idadi ya wanafunzi waliofaulu kujiunga na kidato cha kwanza Januari 2024 imeongezeka kwa wanafunzi 16,947 sawa na ongezeko la asilimia 1.57 ikilinganishwa na wanafunzi 1,076,037 waliopata alama za kuwawezesha kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2023.” Amesema Mchengerwa.
Amesema miongoni mwa waliofaulu na kupangiwa kujiunga na Kidato cha Kwanza Januari, 2024 wamo wanafunzi wenye mahitaji maalum 3,587 ambapo wasichana 1,590 na wavuala 1,997.
WALIOCHAGULIWA KIDATO CHA KWANZA BONYEZA HAPA
from Author
Post a Comment