Angola Walicheza Kiume Sana |Shamteeblog.

Angola waliingia na muundo wa 3-4-2-1 lengo likiwa

1.Kuwaacha mpira Algeria
2.Kuzuia kwa idadi kubwa bila mpira
3.Kusubiri kushambulia kwa transit

Angola kipindi cha kwanza bila mpira walikuwa wanazuia kwenye muundo wa 5-4-1.Angola kwenye muundo huu wa kuzuia ilikuwa wakipata mpira walikuwa wanashambulia kwa namba ndogo sana

Kocha Soares Goncalves wa Angola aligudua timu ikiwa inazuia kwenye muundo wa 5-4-1 ilikuwa inakosa uwiano kwenye kipindi cha kushambulia hasa kipindi Cha mpito.

Kwa hiyo Soares alichokifanya ni kubalisha mfumo wa timu kutoka kwenye 3-4-2-1kwenda kwenye 4-4-2,Katika kubadilisha mfumo alimuingiza Mabululu kwa ajili ya kuongeza matendo ya kiushambuliaji kwenye box la mwisho la Angola(Offensive Actions)

Angola kwenye muundo wa 4-4-2 walicheza sana kwasababu

1.Wakati wanashambulia walitengeneza muundo 2-4-4 hasa kwa kushambulia channels za pembeni mwa uwanja

2.Angola kwenye muundo wa 4-4-2 walifaidika na jinsi ambavyo mabululu alikuwa anawapa shida mabeki wa kati wa Algeria.

Angola kwenye huu muundo 4-4-2 bila mpira walibadilika na kuzuia kwenye 5-4-1 hasa kipindi cha pili dakika za mwisho.

Angola kwenye 5-4-1 walifanya vitu vya msingi sana

1.Walikimbia sana uwanjani
2.Walikuwa wanapress vizuri kuanzia katikati mwa uwanja
3.Walizuia vizuri maeneo ya juu yaani aerial space

Kuna muda ilifika Algeria ilibidi watengeneze 10 vs 10 na Angola kwenye kipindi Cha kushambulianlakini bado ilishindika kupata goli.

Zingatia

Mabululi what a player ,kwa kiasi kikubwa alibadilisha sana mchezo

Yule beki wa kati wa Angola Kialonda Gaspar
1.Anajua kupiga pasi
2.Anajua kucheza mipira ya juu
2.Anacheza kizalendo sana kafanya kazi chafu.

Adilson Neblu Kipa Angola alihakikisha sare ya 1-1 inapatikana.

Soares kocha wa Angola aliheshimu quality ya Algeria 📌

Full-time
Algeria 1-1 Angola

✍ @omarrkombo

The post Angola Walicheza Kiume Sana appeared first on Kitenge Blog.



By Author

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post