Kamati: Mwamuzi alikosea kuwapa Simba kona |Shamteeblog.

Mpira wa kona uliopigwa na Simba dakika za lala salama na kupelekea goli la kusawazisha lililofungwa na Fabrice Ngoma haukuwa sahihi.

Hata hivyo, mwamuzi huyo Nasri Salum, maarufu Msomali hatopewa adhabu zaidi ya onyo kwa sababu makosa ni sehemu ya binadamu, kamati ya waamuzi ya Zanzibar imesema.

Kamati hiyo imeyasema haya baada ya kikao chake kujadili tukio hilo lililoleta mjadala katika mitandao ya kijamii.

Mwenyekiti wa kamati hiyo Waziri Shekha amenukuliwa akisema mwamuzi huyo hakuwa sahihi kwa kona hiyo, lakini alikuwa sahihi katika matukio mengine ya mchezo huo.

” Tulibaini amekosea,lakini makosa ni sehemu ya ubinadamu, hivyo tumempa onyo,” amesema.

Kona hiyo ilipelekea Simba kusawazisha ndani ya dakika za nyongeza na kupelekea mchezo huo wa Nusu Fainali dhidi ya Singida Big Fountain kwenda katika matuta na Simba kuibukia washindi na kwenda fainali ambapo watacheza dhidi ya bingwa mtetezi Mlandege.

The post Kamati: Mwamuzi alikosea kuwapa Simba kona appeared first on Kitenge Blog.



By Author

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post