Tanzania Tumecheza Ovyo Sana, Tumefungwa Mabao Matatu Hatuna Hata Short On Target Moja, Tubadilike |Shamteeblog.



Pamoja na kuwa tumecheza na timu bora sana namba moja Barani Africa na kiukweli wamewekeza sana kwenye soka lao kuliko sisi lakini tumecheza hovyo sana chini ya kiwango approach ya mwalimu Adel Amrouche ya mfumo wa 5-2-3 haikumlipa pamoja na kucheza watu 9 nyuma ya mpira kwenye low block lakini bado Morocco 🇲🇦 wameweza kuifungua Deffensive zone yetu na kutengeneza nafasi za kutosha na kisha kuzitumia kuzalisha mabao ya kutosha.

Namna ambavyo tulikuwa tunacheza hapakuwa na pattern iliyotengenezwa bora ya ushambuliaji mbele kwenye eneo la 14 zones tulikuwa hatufiki mara nyingi waliweza kutu press kwa juu sana na kutokutupa nafasi ya kuingia kwenye eneo lao la 1/3 ya zone yao kirahisi na wakafanikiwa kwa hilo.

Kwangu mimi Bwana Samata hakupaswa kutoka isipokuwa alipaswa kuongezewa watu wa kucheza naye mechi ya leo ilikuwa inamuhusu sana Kibu Denis kwakuwa ana nguvu anaweza kukimbia Sana na ana uwezo mkubwa wa kukaba.

Aishi anapaswa kubadilika aina yake ya uokoaji wa mipira wengi mnabisha juu ya hili kama mmemtazama sana anaokolea sana kwa kutemea mipira ndani kidogo azalishe goli lingine tena la aina hiyo hiyo ya kutemea ndani.

Baadhi ya wacheza wa Taifa stars wamekosa kabisa hali ya upambanaji na kuonekana hawana kabisa mpango kazi wakati timu ikiwa inacheza.

Mwalimu Adel Amrouche ana kazi kubwa sana ya kufanya kwa michezo iliyobakia ukizingatia Stars yupo kwenye kundi gumu sana.

FT: MOROCCO 🇲🇦 3 VS TANZANIA 🇹🇿 0


from Author

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post