KATAMBI: KIWANGO CHA PENSHENI YA KILA MWEZI KWA WASTAAFU KIMEBORESHWA |Shamteeblog.

 

NAIBU Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe.Patrobas Katambi, akijibu swali la Mbunge wa Segerea (CCM), Mhe.Bonnah Kamoli leo Februari 5,2024 bungeni jijini Dodoma.

Na Mwandishi Wetu, DODOMA

NAIBU Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe.Patrobas Katambi amesema katika kanuni mpya ya mafao iliyoanza kutumika Julai mosi 2022, serikali iliboresha kiwango cha mafao ya pensheni ya kila mwezi kwa wastaafu kutoka asilimia 50 hadi 67.

Mhe.Katambi ameyasema hayo Februari 5, 2024 bungeni jijini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Segerea (CCM), Mhe.Bonnah Kamoli ambaye amehoji lini kanuni mpya za malipo ya pensheni kwa wastaafu ya kila mwezi ya kutoka asilimia 50 hadi 67 itaanza kutumika.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri Katambi amesema kupitia gazeti la serikali namba 357 la Mei 20, 2022 ilitangaza kanuni hiyo iliboresha kiwango cha mafao ya pensheni ya kila mwezi kwa wastaafu.

Amesema kanuni hizo ziliandaliwa kwa kushirikisha wadau wote (Serikali, Wafanyakazi na Waajiri) kwa lengo la kufanya maboresho ya pensheni ili kuwianisha mafao ya wanachama na kuifanya mifuko kuwa endelevu.



By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post