MPANGO WA RAIS DKT SAMIA NI KUUNGANISHA BANDARI YA TANGA NA RELI ILI KUPUNGUZA MSONGAMANO KATIKA BANDARI YA DAR -PROFESA KAHYARARA |Shamteeblog.





KAIMU Meneja wa Bandari ya Tanga Peter Milanzi kushoto akimuonyesha kitu KATIBU Mkuu Wizara ya Uchukuzi Profesa Godius Kahyarara wakati alipofanya ziara ya kutembelea Bandari ya Tanga



KATIBU Mkuu Wizara ya Uchukuzi Profesa Godius Kahyarara katikati akimueleza jambo Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga Peter Milanzi wakati alipofanya ziara ya kutembelea Bandari ya Tanga



KATIBU Mkuu Wizara ya Uchukuzi Profesa Godius Kahyarara katikati akimueleza jambo Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga Peter Milanzi wakati alipofanya ziara ya kutembelea Bandari ya Tang





Na Oscar Assenga, Tanga.


KATIBU Mkuu Wizara ya Uchukuzi Profesa Godius Kahyarara amesema mpango wa Rais Dkt Samia Suluhu ni kuunganisha Bandari ya Tanga na Reli ili kurahisisha utoaji wa shehena ya mizigo kwenda maeneo mbalimbali nchi ikiwemo mikoa ya Kaskazini na hivyo kupungunza msongamano kwenye Bandari ya Dar es Salaam.

Kiharara aliyasema hayo leo wakati alipofanya ziara ya kutembelea Bandari ya Tanga kujionea maboresha makubwa yaliyofanywa na Serikali ambapo alisema ili kuunganisha Bandari na Reli katika mkoa huo kuna mradi maalumu wa kuchepusha reli ya kaskazini wenye urefu wa kilomita 435 inayokwenda mikoa ya kaskazini ikitoka Dar kupitia Tanga.

Alisema kwamba tayari serikali imekwisha kutoa fedha na wamekwisha kuanza kubadilisha vyuma njia ya treni ili iweze kuhimili spindi kuongezeka ambapo mradi huo utakamilika muda mfupi na itawezekana kuchukua mizigo kutoa Tanga kwenda Dar es Salaam.

“Mradi huu utakwenda kufufuliwa kwa haraka kwa maana fedha tayari wamekwisha kupewa na matumaini yetu Bandari ya Tanga itakuja kuisaidia Bandari ya Dar es Salaam na tumeona Bandari ya Tanga hawajaitumia ipasavyo kwani ina uwezo wa kupitisha tani milioni 3 na Bandari ya Mtwara ni ndogo kuliko ya Tanga lakini inapitisha mizigo mingi hivyo tunaona ni changamoto lazima tuwasaidie wenzetu wa Tanga kwanza wajitangaze”Alisema

“Tusiangalie Tanga kwa vitu vinavyotoka hapa kama zao la Mkonge na mengine lakini Tanga ina muunganiko na Dar es Salaam ndio maana tunaimarisha reli kwani inaweza kuchukua masaa manne kutoka Tanga hadi Dar”Alisema

Katibu huyo alisema inawezekana mtu mwenye bidhaa zake akitaka kuzifikia Dar akipitisha Tanga iwe ni rahisi kuifika Dar na maboresho hayo yanataka kuunganisha Bandari ya Tanga na mfumo wa reli ya kati inayoanzia Ruvu kuelekea Isaka hivyo ukiwa na mzigo unataka kwenda huko itakuwa ni rahisi sana kwamba kwa spidi itakayokuwa imeongezeka kutoka Dar mpaka Isaka.

Alisema kutokana na maboresho hayo makubwa hivyo mpango wa serikali wa kuunganisha Bandari hizo utakuwa umefanikiwa baada ya kukamilika kwa maboresho hayo treni inaweza kutembea spidi angalau 70 hadi 80 lakini sasa sehemu kubwa ya reli ni mbovu na hivyo kupelekea treni kwenda taratibu hivyo maboresho hayo yatasaidia kuondoa hilo”Alisema

Kutokana na hilo itasaidia kuiwezesha Bandari ya Tanga kutumika kuisaidia Bandari ya Dar es Salaam kuliko kukaa foleni ya wiki nzima kwani masaa ya kutoka Tanga hadi Dar sio mengi sana kuna mizigo wanaweza kusema iteremkie Tanga ikiwemo ile maalumu na hivyo kupunguza msongamano kwenye Bandari ya Dar.

Awali akizungumza wakati wa ziara hiyo Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga Frank Milanzi amesema uwekezaji uliofanyika kwenye Bandari ya Tanga umesaidia kuifungua kibiashara Bandari hiyo kutokana na kuweza kuhudumia meli nangani ikiwemo mizigo kutoka nchi jirani

“Kwa kweli tunaishukuru Serikali kwa kazi kubwa iliyofanyika hivi sasa tunapokea meli mpana gatini na hivyo kupunguza gharama ambazo wateja walikuwa wanaipata awali”Alisema Milanzi

Kwa upande wake Katibu Mkuu, Wizara ya Uchukuzi, Mawasiliano na Usafirishaji kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Khalifa Khamis Rajab amesema lengo la mkutano huo ni kuendeleza ushirikiano baina yao kwakuwa kazi inayotekelezwa ni moja katika kuwahudumia wananchi.

“Tumekuja hapa kuendeleza ushirikiana baina yetu kwa kuwa kazi inayotekelezwa ni mojakatika kuwahakikisha tunawahudumia wananchi”Alisema

Hata hivyo Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga Peter Milanzi amesema kwamba wana matarajio makubwa ya kufunguka kwa Mkoa wa Tanga kupitia bandari hiyo ikiwemo mradi wa uboreshaji ambao umekamilika mwishoni mwa mwaka uliopita.

Alisema kutokana na maboresho hayo makubwa yaliyofanywa katika Bandari hiyo yameiwezesha kuanza kupokea oda za makampuni makubwa kutoka nje ya nchi .


By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post