WANASIASA, WATUMISI NA WANANCHI KUPEWA ELIMU KUKABILIANA NA VITENDO VYA RUSHWA KWENYE UCHAGUZI |Shamteeblog.

Na Hamida Kamchalla, TANGA.

TAASISI ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Tanga imejipanga kimkakati kuwafikia na kuwapa elimu viongozi na wanachama wa vyama vya siasa, watumishi na makundi yote katika jamii katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi.

Watumishi watakaofikiwa ni wale wanaouhusika na mchakato wa uchaguzi ili wapiga kura na wadau wa uchaguzi watambue athari za vitendo vya rushwa na wachukue hatua za uzuiaji wanapoona dalili za kutendeka kwa vitendo hivyo.

Kwa niaba ya Mkuu wa TAKUKURU mkoani hapa, Frank Mapunda amesema wanaendelea programu ya TAKUKURU Rafiki katika kata mbalimbali ili kuongeza ushiriki wa kila mwananchi katika kuzuia vitendo vya Rushwa, utoaji huduma kwa jamii pamoja na utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

"Tunaendelea kufanya udhibiti na uzuiaji rushwa kwenye eneo la ukusanyaji mapato kwa kushirikiana na mamlaka husika kufanya ufuatiliaji wa moja kwa moja kwenye vyanzo vilivyoainishwa katika bajeti,

"Hii ni katika kuangalia mienendo ya makusanyo ya mapato sambamba na kushauri hatua mbalimbali za kudhibiti upotevu wa mapato wakati wa mchakato wa ukusanyaji" amesema.

Pia amesema wataendelea kufanya ufuatiliaji wa matumizi ya rasilimali za umma hususani katika utekelezaji wa miradi kwenye sekta ya Elimu miradi ya BOOST na SEQUIP.

Lakini pia ni pamoja na miradi inayotekelezwa na RUWASA na TANGA Uwasa na kushauri hatua madhubuti kuchukua ili kudhibiti ubadhirifu na ufujaji unaweza kufanyika wakati wa utekelezaji wa miradi hiyo.

Amebainisha kwamba, "Kwa kipindi hiki kuelekea kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa, popote mwananchi ulipo, timiza wajibu wako kwa kutojihusisha na vitendo vya rushwa kwa kuomba wagombea au sehemu ya kutoa rushwa kwa wanachama".

Vilevile amesema katika utekelezaji wa Program Rafiki wameshazifikia kata 24 ambapo jumla ya kero 199 zimeibuliwa na kuchambuliwa, kati ya kero hizo 11 zipo katika hatua mbalimbali za utatuzi.

Mapunda amesema ushirikiano wa wadau katika program hiyo uko imara hasa kwa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Sekretarieti yake, Ofisi ya wakuu wa Wilaya na Sekretarieti zake na wadau wote kwenye Taasisi za umma na binafsi pamoja na makundi ya wananchi wote.


"Tumeshirikiana na wadau hawa kwa pamoja katika uelimishaji na uhamasishaji uzuiaji vitendo vya rushwa, uchambizi wa mifumo na ufuatiliaji utekelezaji wa miradi ya maendeleo, na tunaomba ushirikiano huu undelee' amesema.



By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post