RAIS SAMIA AIPONGEZA WIZARA YA MADINI KWA USIMAMIZI MADHUBUTI WA SEKTA |Shamteeblog.


⚫️ Trilioni moja yatengwa kwa ajili ya ununuzi wa dhahabu kupitia BOT

● Shilingi Bilioni 250 zatengwa kama dhamana ya mikopo kwa wafanyabiashara wa dhahabu

●Mwaka 2023 madini yenye thamani zaidi Trilioni mbili yaliuzwa kupitia masoko

●Serikali kuongezea mitambo ya uchorongaji 10 zaidi kwa ajili ya wachimbaji wadogo

GEITA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia  Hassan ameipongeza wizara ya madini kwa usimamizi mzuri na  madhubuti wa sekta ya madini unaopelekea ukuaji wa haraka na kuwa kinara katika  kuchangia kwenye Pato la Taifa.

Hayo yameelezwa leo Oktoba 13, 2024 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan wakati akifunga maonesho ya Saba ya Teknolojia ya Madini mkoani Geita.

Aidha Mh Rais Samia ameeleza katika mikakati ya kuimarisha uchumi wa nchi na upatikanaji wa fedha za kigeni Serikali kupitia Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imetenga kiasi cha shilingi Trilioni moja kwa ajili ya ununuzi wa dhahabu  kutoka kwa wachimbaji.

Rais, Dkt. Samia amesema kwamba  sekta ya madini imekuwa na mchango mkubwa katika kuliingizia taifa fedha za kigeni ambapo kwa mwaka wa fedha 2022/2023 ilichangia asilimia 56 ya fedha za kigeni.

Sambamba na hapo Rais , Dkt.Samia amesema kiasi cha shilingi 250 zimetengwa kama dhamana ya mikopo zitakazo wawezesha wanunuzi wa dhahabu kupata mtaji.

Rais Dkt. Samia amesema kuwa ,  kwa mwaka wa 2023 mauzo ya madini yenye thamani ya zaidi ya shilingi trilioni mbili yaliuzwa katika masoko 44 na vituo mbalimbali vya uuzaji madini  vilivyopo sehemu mbalimbali nchini.

Akielezea kuhusu mwenendo wa biashara ya madini nchini kuanzia mwaka 2019 mpaka septemba 2024 , Dkt.Samia amesema kwa kipindi husika kiasi cha tani 20.8 za dhahabu zenye gharama ya shilingi trilioni 5.2 zimenunuliwa kutoka kwa wachimbaji na wafanyabiashara ya madini nchini.

Dkt.Samia ameeleza serikali inatambua mchango wa asilimia 40 kutoka kwa wachimbaji wadogo nchini, ambapo ametoa leseni 21 kwa vikundi vya Vijana na wanawake  vikiwemo vikundi vya GEWOMA , Ushirika Madirisha na TEWOMA vinavyojihusisha na uchimbaji mdogo.

Naye , Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati , Dkt.Dotto Biteko ameipongeza wizara ya madini kwa juhudi mbalimbali inazofanya za mageuzi katika mnyororo wa thamani katika sekta ya madini hususan katika masuala uongezaji thamani madini na mpango ya kufanya utafiti wa kina kwa asilimia 50 ifikapo mwaka wa 2030.

Akielezea kuhusu mikakati iliyopo  ndani ya sekta ya madini , Waziri wa Madini , Mhe. Anthony Mavunde amesema katika kuimarisha uchimbaji wenye tija na uhakika Serikali itajenga Maabara kubwa mkoani Dodoma na Geita ili
 kuwawezesha wachimbaji wadogo kupeleka sampuli zao kwa ajili ya  uchunguzi wa sampuli za madini na miamba.

Waziri Mavunde amesema kuwa, wizara inaendelea kuweka mipango mizuri katika ukusanyaji wa maduhuli ambapo kwa kipindi cha siku 90 cha mwaka wa 2024/2025 wizara kupitia Tume ya Madini imekusanya kiasi cha shilingi Bilioni 287 ambayo ni zaidi ya asilimia 106.

Akielezea kuhusu utekelezaji wa Sheria na Kanuni ndani ya Wizara, Waziri Mavunde amesema kuwa  wizara imekuwa ikizingatia taratibu zote za  utekelezaji wa Mpango wa Ushirikishwaji wa Jamii inayozunguka mgodi na Mpango wa Urudishaji kwa Jamii ambapo kwasasa ipo  na mpango mpya wa Mining for Brighter Tommorrow (MBT) utakao washirikisha vijana na wakina mama.

Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Geita Mjini Mhe. Constantine Kanyasu amemshukuru  Rais , Dkt.Samia kwa kupeleka fedha za miradi ya  maendeleo mkoani Geita katika sekta ya Afya,Maji, Barabara na  Elimu.

Pamoja na mambo mengine , Rais wa Shirikisho la Wachimbaji wadogo wa madini Tanzania (FEMATA) John Bina amemuomba Rais , Dkt. Samia kuifanya dira ya Vision2030 ya Madini ni Maisha na Utajiri kuwa kitaifa badala ya kisekta.



By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post