NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limewataka wafanyabiashara kutumia teknolojia na kuongeza ubunifu unaozingatia kanuni za ubora wa bidhaa ili waweze kushindana katika masoko ya kimataifa .
Wito huo umetolewa leo Novemba 13, 2024 Jijini Dar es Salaam, na Meneja wa Ithibati ubora wa bidhaa TBS, Amina Yassini wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Maadhimisho ya Wiki ya Ubora ambayo hufanyika kila wiki ya pili ya mwezi novemba.
Amesema msingi wa ubora lazima uzingatie kanununi za ubora ili kukuza masoko na kuongeza ushindani
"Watendaji wanapaswa kuongezewa ujuzi kwa kupata fursa ya kuhudhuria mafunzo kwenye midahalo hii nayo itatusogeza". Amesema
Aidha Amina amewataka wazalishaji wa bidhaa kuzalisha bidhaa ambazo hazitaleta madhara ya kimazingira na kuathiri mabadiliko ya hali ya hewa kwa lengo la kulinda vizazi vijavyo.
Amesema miongoni mwa shughuli zitakazofanywa kupitia maadhimisho hayo ni pamoja na kutoa elimu kwa wadau juu ya kusimamia ubora wa bidhaaa pamoja na utoaji wa tuzo za kutambua taasisi, wafanyabiashara na mtu binafsi wenye mifumo thabiti ya ubora
Amebainisha kuwa wanatarajia kutangaza majina ya washindi kwenye vipengele vitano vya tuzo ya ubora ambapo walipokea maombi kwa mwezi mmoja wa Agosti 2024 kwenye vipengele mbalimbali ambavyo ni mtoa huduma bora wa mwaka, bidhaa bora ya mwaka, huduma bora ya mwaka, muuzaji bora wa bidhaa nje ya nchi na mtu mwenye mchango wa kujenga Mifumo bora ya ubora wa bidhaa.
Kilele cha Maadhimisho hayo kimebeba kauli mbiu isemayo UBORA KWA KUZINGATIA MATAKWA YA VIWANGO HADI KWENYE UTEKELEZAJI ambapo yatafanyika Novemba 18,katika Ukumbi wa PSSF unaopatikana barabara ya Sam Nujoma na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Seleman Jafo.
By Mpekuzi
Post a Comment