Rais Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za pole kwa familia ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali mstaafu, Jaji Frederick Werema, huku akiwataka kuwa na subira na imani kufuatia kifo cha nguli huyo wa sheria nchini.
“Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha
Mwanasheria Mkuu wa Serikali mstaafu, mheshimiwa Jaji mstaafu Frederick Werema.
Ninatoa pole kwa familia, mheshimiwa Jaji Mkuu, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Majaji, ndugu, jamaa na marafiki”
“Nawaombea kwa Mwenyezi Mungu awajalie subra na imani katika kipindi hiki cha kuomboleza msiba huu, na ailaze roho ya mpendwa wetu huyu mahali pema peponi,”- amesema.
Rais Samia ametuma salamu hizo kupitia mitandao yake ya kijamii leo Jumatatu, Disemba 30, 2024, muda mchache tangu kutolewa kwa taarifa za kifo cha Jaji mstaafu Werema zilipoanza kusambaa mitandaoni.
By Mpekuzi
Post a Comment