THE BLESSED PRAISE AND WORSHIP TEAM KUFANYA MAAJABU KAGERA KUFUNGA MWAKA 2024! |Shamteeblog.

 

Na Lydia Lugakila -Bukoba.

Tamasha  kubwa na la aina yake linataraji kunguruma Desemba 29,2024 saa nane mchana katika Viwanja vya Bukoba Sekondari lengo likiwa ni kumsifu Mungu na Kumwabudu na Kumshukuru kwa ajili ya mwaka huu 2024.

Akizungumza na Malunde 1 blog mmoja wa  walezi wa kikundi hicho Pastor Agape kutoka kanisa la Kinabii  ECG Taifa la Yesu mjini Bukoba alisema kuwa kikundi cha The Blessed Praise and Worship kitakuwa kinatambulisha nyimbo zao kadhaa katika ibada hiyo ya fungua malango ya Mbinguni ambapo ametumia fursa hiyo kuwaomba wazazi kuwapeleka watoto wao kujifunza namna ya kumwabudu na kumsifu Mungu kupitia uimbaji.

Kiongozi wa Kikundi hicho Elgibo Emmanuel ametumia fursa hiyo pia kuwakaribisha Wananchi wote wa Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera na kuwa watu wote watamwabudu na kumsifu Mungu kwa pamoja ikiwa ni pamoja kupokea muujiza mkubwa.

Amesema hakika kila mtu atabarikiwa sana atakapoingia mwaka 2025 kwa kumwabudu na kumsifu aliye juu maana malango ya Mbinguni yatamfungukia kwa ajili mambo makubwa yenye utakatifu wa Mungu yaliyo mbele yao.

Hata hivyo amesema atatumia fursa hiyo kutoa kuwanoa watoto ili wajue kumuomba na kumwabudu Muumba wao.



By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post