THBUB YAENDELEA KUTOA ELIMU YA HAKI ZA BINADAMU NA MISINGI YA UTAWALA BORA KWA WATENDAJI KATA |Shamteeblog.


Ujumbe wa Tume ya Haki za Binadamu  na Utawala (THBUB) ukiongozwa  na Makamu  Mwenyekiti Mhe.Mohamed  Khamis  Hamad,umetoa mafunzo  kwa Watendaji  Kata wa Kata  za Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, leo Januari  27,2025  katika Ukumbi wa Mikutano uliopo katika Ofisi za Halmashauri  hiyo.

Aidha,Mafunzo hayo yamelenga kuwakumbusha Watendaji  namna ya kuzingatia haki za binadamu  na misingi  ya utawala bora wakati utekelezaji  wa majakumu yao ikiwemo ushirikishaji wananchi katika masuala mbalimbali  yanayowahusu

Pia,Watendaji  hao wamepata nafasi ya kuuliza maswali sambamba nakuwasilisha changamoto  wanazokutana nazo wakati wa kutekeleza majukumu yao.


By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post