WAZIRI BASHUNGWA AZINDUA MIKAKATI SITA YA MAWASILIANO KUONGEZA TIJA KWENYE UTENDAJI KAZI |Shamteeblog.



Na Dotto Kwilasa, Dodoma. 

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Innocent Bashungwa amewaelekeza wasemaji wa vyombo vya usalama na wakuu wa vitengo vya habari na mahusiano  kufanya tathmini ya pamoja ya utendaji kazi wa vitengo vya habari katika Wizara na vitengo vyake vya usalama kwa kuzingatia mpango kazi unaosomana.

Bashungwa ameeleza hayo Januari 9,2025 Jijini Dodoma wakati akizindua mikakati Sita itakayotekelezwa  ili kuweze kutimiza lengo na kuimarisha nguvu za kiutendaji na kueleza kuwa  kuzinduliwa kwa mikakati hiyo kunapaswa kuwa chachu ya kuitekeleza kwa ufanisi ili ilete tija kwa Wizara kwani itasaida kuimarisha suala la Mawasiliano kwa umma.

"Hakikishe kuwa vitengo vyetu vya habari vinatengewa bajeti ili viweze kutelekeza mikakati hii ya mawasiliano kwani inaleta tija na mabadiliko chanya kwenye kuwahudumia watanzania,"amesema. 

Amesema miongoni mwa malengo ya kuangaliwa kwenye mikakati hiyo ya mawasiliano ni kuongeza uelewa na ushiriki wa jamii kwenye kuimarisha usalama wa raia na mali zao sambamba na utunzaji wa amani na utulivu wa nchi. 

Naye Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Daniel Sillo amewahasa washirki kikao kazi cha mwaka cha wasemaji wa vyombo vya usalama na maafisa habari, Mawasiliano na uhusiano wa Wizara hiyo kutumia jukaa hilo kijtathmini walipotoka, walipo na wanakoeleea ili kwa pamoja waweze kupata uzoefu ambao utasaidia kuimarisha sekta ya habari kwa maslahi ya wananchi na taifa kwa ujumla. 

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Ally Gugu amesena mikakati hiyo inasaidia kuboresha upatikanaji wa habari ambayo ndiyo lengo la Serikali ya awamu ya sita ili kuiwezesha jamii kupata taarifa kwa wakati ambapo ni mapendekezo ya tume ya haki jinai.

"Katika kutekeleza maelekezo ya Serikali Wizara yetu imeanza na uandaaji wa mikakati hii ya mawasiliano ambayo imezinduliwa leo na baada ya hapo tutaenda kuitekeleza kwa vitendo na kwakuwa zipo shughuli mbalimbali ambazo zimepangwa kutekelezwa kwa miaka miwili na baada ya hapo tumepanga kufanya mapitio ili kuona hatua mbalimbali za utekelezaji wa mikakati hiyo, "amesema. 

Awali akitoa taarifa kuhusu mikakati hiyo Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini  Christina Mwangosi amesema mikakati hiyo imeandaliwa kwa kuzingatia miongozo ya Wizara, vyombo ya usalama pamoja na mkataba wahuduma kwa wateja.

"Mikakato hii ni ya miaka mwili na baada ya hapo tutafanya tathmini ya matokeo yatakayokuwa yamepatikana na ndipo tutaanza tena mikakati mingine kulingana na matokeo yatakayokuwa yamepatikana,"amesema.

Hata hivyo Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imezindua Mikakati Sita ya mawasiliano yenye lengo la kuimarisha upatikanaji wa huduma kwa urahisi kwenda kwa wananchi. 





By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post