KATIBU UWT CHINYOYO,KATA YA KILIMANI AFUNGA NDOA |Shamteeblog.



Na Barnabas Kisengi, Malunde Blog Dodoma.

Ni siku ya shangwe na nderemo na vifijo isiyosahauka kwa katibu wa Umoja wa Jumuiya wa wanawake Tanzania UWT CCM Tawi la chinyoyo kata ya kilimani Jijini Dodoma Bi Domina Kiria kufunga pingu za maisha na bwana Godfrey Mwasi February 15. 2025 .

Ndoa hiyo takatifu imefungwa katika kanisa katoliki la Mt. Paulo wa Msalaba Jimbo kuu la Dodoma na kufuatiwa na tafrija ya kuwaongeza maharusi hao iliyofanyika katika ukumbi wa Ulanga hotel Jijini Dodoma.

Akizungumza na Malunde Blog Jijini Dodoma Mara baada ya kiapo hicho cha ndoa Katibu huyo amewaasa vijana kuhalalisha mahusiano yao ili kuenenda kwenye njia nyoofu.

"Natambua ndoa ni baraka,kabla hujaingia kwenye ndoa ni lazima umpate mtu unayefanana naye, anayekubali mapungufu yako wakati wote na hapo unaweza kufurahia siku za maisha ambazo mwenyezi Mungu amekujalia, " amesema










By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post