MBUNGE MSHASHU AMPONGEZA RAIS SAMIA KWA UTENDAJI ULIOTUKUKA |Shamteeblog.



Na Lydia Lugakila- Bukoba

Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Kagera Bernadeta Kasabago Mshashu amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Dkt. Samia Suluhu hassan kwa jinsi alivyoupendelea Mkoa huo na kuupatia Mabilioni ya pesa ambayo yameuwezesha Mkoa huo kuwa na maendeleo makubwa kiuchumi  pamoja na kuiongoza Nchi kwa umakini mkubwa.

Mshashu ametoa kauli hiyo katika kikao cha kamati ya ushauri ya Mkoa -RCC kilichofanyika Februari 19,2025 katika ukumbi wa Mkoa huo.

"Tumeona kazi kubwa aliyoifanya Rais wetu tumeona miradi mingi ya kimkakati   tunampongeza Rais Samia hakika ametuheshimisha Kagera"alisema mbunge huyo.

Mshashu Amempongeza pia Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Hajat Fatma Mwassa kwa usimamizi imara katika miradi mbali mbali ya maendeleo Mkoani humo huku akiwapongeza pia  wakuu wa Wilaya pamoja na watendaji mbali mbali ambao wemeweka juhudi zao katika kuuinua Mkoa huo ki uchumi.

Hata hivyo kiongozi huyo amewaomba Wanakagera na Watanzania kumuombea Afya njema Rais Samia ikiwa ni pamoja na kumpigia kura za Kishindo kwa uchaguzi mkuu ujao Mwaka huu.




By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post