Na Lydia Lugakila - Kyerwa
Meneja wa Azania Bank tawi la Rockcity Mall, Mkoani Mwanza Bi Bernadeta Makigo amezikaribisha AMCOS zote zilizopo Mkoa wa Kagera na maeneo mengine kuijaribu benki hiyo ki huduma kwani ni benki inayotoa kinahitajiwa na mteja kwa wakati lengo likiwa ni kuwawezesha kununua zao la Kahawa kwa Wananchama wake na kujiinua ki uchumi.
Makigo ametoa kauli hiyo katika mkutano Mkuu wa kawaida wa Wanachama uliofanyika Marchi 12,2025 katika eneo la kiwanda cha kukoboa Kahawa kilichopo Rubwera wilayani Kyerwa Mkoani Kagera.
Makigo amesema kwa mwaka huu wamejikita sana kwa Wilaya za Karagwe na Kyerwa kwa ajili ya kuwafikia Wakulima na AMCOS zinazoendesha zao la Kahawa.
Aidha ameongeza kuwa benki hiyo ina wateja wao ambao walishafunguliwa akaunti zaidi ya 2000 kwa mwaka 2024 na walikopesha AMCOS moja kwa ajili ya kununua Kahawa na kiasi walichoambiwa hawakuwapunguzia wala kuwaongezea.
Amesema kuwa kwa Mkoa wa Kagera wao walianza kuingia na kujitangaza katika Wilaya ya Karagwe na Kyerwa tangu mwaka 2019 ambapo walitoa huduma mbalimbali za kufungua akaunti na huduma nyinginezo.
"Kuna AMCOS kama za tumbaku zilizoko Tabora walipata changamoto ambapo tumbaku iliungua lakini bima walifidiwa kutokana na kuwa na bima amesema Makigo.
Akiielezea benki ya Azania amesema ni Benki ya Wananchi wote kwa sababu inamilikiwa na mifuko mbali mbali ya hifadhi ya jamii ikiwemo PSSSF, NSSF, NHIF, WCF, EADB na Wananchi hivyo mtu unapoenda kutibiwa hospitali au unapochangia wafanyakazi wako au kulipia ada yoyote ujue unaiwezesha benki hiyo kuendelea.
"Tuna mikopo kwa ajili ya wafanyabiashara mbali mbali, mikopo ya kilimo, mikopo ya wastaafu, mikopo kwa ajili ya ujenzi wa nyumba na mikopo kwa Watumishi wa umma" amesema Meneja huyo.
Hata hivyo amezikaribisha AMCOS zote kuijaribu benki hiyo ili kuona watakavyowahudumia kwa wakati ili waweze kununua zao la Kahawa kwa Wananchama na kuwa kwa mwezi Juni mwaka 2024 walitoa huduma kwa AMCOS 3 katika Wilaya ya Kyerwa na Rockcity walitoa 1 na walifurahi kununua Kahawa kutoka kwa Wanachama wao huku akiomba kuwa wakitumia taasisi nyinginezo za kifedha kuomba mkopo wasisite kuitumia benki hiyo.
By Mpekuzi
Post a Comment