
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Mkutano wa Misa Tanzania na wadau (MISA-TAN - Wadau Summit 2025) itakayofanyika Machi 14, 2025, jijini Dodoma. Kongamano hili linaloandaliwa na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika Tawi la Tanzania (MISA - TAN), litawakutanisha waandishi wa habari na wadau wa habari na mawasiliano kutoka maeneo mbalimbali nchini.

By Mpekuzi
Post a Comment