RC TANGA ATAKA TIMU YA WADAU WA BAHARI KUNOLEWA IPASAVYO KUDHIBITI UVUJAJI MAFUTA |Shamteeblog.

Na Hadija Bagasha Tanga,

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Balozi Dkt. Batilda Salha Burian ametaka timu ya wadau wa bahari wa Mkoa huo kunolewa ipasavyo ili kuwa na uwezo wa kukabiliana na majanga ya uvujaji wa mafuta baharini katika kipindi hiki ambacho Mkoa huo unatarajia kuwa na mradi mkubwa wa bomba la mafuta ghafi kutoka Ohima Nchini Uganda hadi Chongoleani Jijini Tanga. 

 Pia Balozi Dkt Batilda amelipongeza Shirika la Uwakala wa Meli TASAC  kwa kuhakikisha kunakuwa na upatikanaji wa vifaa vya kukabiliana na umwagikaji wa mafuta baharini.  

Kauli ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga anaitoa katika kipindi ambacho mradi mkubwa wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima Uganga hadi Chongoleani jijini Tanga ukiwa umefikia hatua nzuri ya ujenzi. 

Akizungumza kwenye warsha ya mafunzo juu ya mpango wa Taifa wa kujiandaa na kupambana na umwagikaji wa mafuta kwenye bahari na maziwa inayofanyika kwa siku tatu Mkoani Tanga yaliyoandaliwa na TASAC kwa wadau kutoka Tanga na Zanzibar. 

Dkt.  Burian alisema kuwa Tanga katika miaka ya hivi karibuni imeshuhudia utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo ambayo sasa inavutia meli kubwa na nyingi katika ukanda wa Pwani ya Tanga.

Aidha amesema kwamba warsha hiyo itasaidia kukabiliana na umwagikaji wa mafuta baharini ambao unaweza ukasababisha madhara makubwa hata kwenye kilimo cha mwani na viumbe wengine wa majini. 

Akizungumzia maendeleo ya mradi wa mafuta wa Hoima Uganda  hadi Chongoleani,  Mkuu huyo wa Mkoa amesema Bandari ya Tanga kupitia eneo la Chongoleani inatarajiwa kuwa lango kuu la kupokelea  na kupitisha mafuta ghafi hivyo mpango wa kutengeneza timu ya dharura ya kukabiliana na uvujaji wa mafuta majini ni muhimu. 

"Maendeleo kama haya yanamaanisha kuwa licha ya kutoa fursa nyingi za kiuchumi pia inaashiria hatari kubwa ambayo inawataka wadau kuwa tayari kwa tukio lolote la maafa ya umwagikaji wa mafuta," Dkt.  Burian alisema. 

DKT Batilda amesema Mkoa huo tayari umeshajikita kwenye kilimo cha mwani na kwamba kama hakutakuwa na timu ya kulabiliana na majanga ya uvujaji wa mafuta wakulima wa mwanani wanaweza kuwa wahanga wakubwa wakati yanapoweza kutokea majanga yacaina hiyo katika habari ya hindi Tanga. 

Mkuu huyo wa mkoa ameongeza kuwa mbali na madhara ya uvujaji wa mafuta ghafi, viumbe wa majini kama vile samaki navyo vinaweza kuathirika sambamba na binadamu wanaotegemea rasilimali bahari kwa kiwango kikubwa. 

Aidha alizitaka Halmashauri za Serikali za Mitaa kutengeneza mipango yao ya dharura ya upotevu wa mafuta na kuweka bajeti kwa ajili hiyo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Masuala ya Usalama na mazingira baharini Leticia Mutaki amesema warsha hiyo inalenga kujenga timu imara yenye uwezo wa kukabiliana na majanga ya uvujaji wa mafuta. 

Timu hiyo ya wadau mbalimbali wa bahari  inakutana kwa miaka mitatu mfululizo ikijengewa uwezo wa kukabiliana na majanga ya uvujaji wa mafuta baharini pale itakapotokea. 



By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post