WASANII WAPEWA MKOPO WA SHILINGI BILION 5.2 |Shamteeblog.



Na Doto Kwilasa ,Dodoma

Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kupitia sekta ya Utamaduni na sanaa imetoa mikopo yenye thamani ya shilingi Bilioni 5.2 kwa miradi 359 Sanaa iliyozalisha ajira 497213 ikiwemo miradi ya mziki 78, filam 90 ,maonesho 65 ufundi 103 ,lugha na fasihi 23.

Haya yameelezwa na Mtendaji mkuu wa mfuko wa utamaduni na Sanaa Tanzania Nyakaho Mahemba leo jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habar kuhusu mafanikio ya sekta hyo.

Mfuko unatoa mikopo kwa kushirikiana na benki ya CRDB na NBC ambapo lengo la ushirikiano huu ni kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma ,kutumia utalaamu na uzoefu wao katika eneo la utoaji wa mikopo na usimamizi wa marejesho pamoja na ufatiliaji wa miradi inayowezeshwa " Amesema mahemba.

Mwisho mahemba ametaja baadhi ya mikoa 18 iliyonufaika na mikopo hiyo ni Dar es Salaam, Arusha ,morogoro,pwani Geita,mwanza,Mbeya,Dodoma,Kagera, Mara,shinyanga ,Tabora,Singida ,manyara,kilimanjaro,simiyu, kigoma na katavi.


By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post