DC KISHAPU : MAKAMPUNI YA KUNUNUA PAMBA YANAYODAIWA HAYATAPEWA MKATABA WA UNUNUZI MSIMU HUU |Shamteeblog.

Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe.Peter Masindi akizungunza kwenye kikao cha Kujadili maandalizi ya ununuzi wa pamba msimu mpya wa mwaka 2025/2026 katika ukumbi wa Shirecu Mei,14,2025 kilichowakutanisha na wadau mbalimbali wa zao la pamba.

Na Sumai Salum-Kishapu 

Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe.Peter Masindi amekutana na wadau wa zao la pamba katika kikao kilichofanyika Mei 14,2025 ukumbi wa SHIRECU kwa lengo la kujadili maandalizi ya ununuzi wa pamba kwa msimu mpya wa mwaka 2025/2026.

Kikao hicho kimewakutanisha wawakilishi wa wakulima, wanunuzi, viongozi wa vyama vya msingi (AMCOS), maafisa ugani pamoja na wataalamu kutoka taasisi mbalimbali, ambapo masuala muhimu kuhusu bei ya pamba, mizani, ubora wa zao, na changamoto za ununuzi yamejadiliwa kwa kina.

Mhe. Masindi amesisitiza umuhimu wa ushirikiano baina ya wadau wote ili kuhakikisha kuwa mkulima ananufaika ipasavyo na juhudi zake, huku akielekeza kuhakikisha mizani yote inayotumika imethibitishwa na wakala wa vipimo .

“Serikali inataka kuona wakulima wananufaika, na hakuna sababu ya mkulima kudhulumiwa kutokana na uzito usio sahihi au ucheleweshaji wa malipo,” ameongeza Mhe. Masindi.

Ameyakumbusha makampuni yanayodaiwa na Halmashauri hiyo madeni ya misimu iliyopita kulipa fedha hizo hadi ifikapo Ijumaa Mei 16 mwaka huu tofauti na hapo makampuni hayo hayataruhusiwa kununua pamba Wilayani humo kwa msimu mpya wa 2025/2026.

Katibu Tawala Wilayani Kishapu Fatma Mohamed amewataka maafisa ugani 
Na Sumai Salum-Kishapu 

Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe.Peter Masindi amekutana na wadau wa zao la pamba katika kikao kilichofanyika Mei 14,2025 ukumbi wa SHIRECU kwa lengo la kujadili maandalizi ya ununuzi wa pamba kwa msimu mpya wa mwaka 2025/2026.

Kikao hicho kimewakutanisha wawakilishi wa wakulima, wanunuzi, viongozi wa vyama vya msingi (AMCOS), maafisa ugani pamoja na wataalamu kutoka taasisi mbalimbali, ambapo masuala muhimu kuhusu bei ya pamba, mizani, ubora wa zao, na changamoto za ununuzi yamejadiliwa kwa kina.

Mhe. Masindi amesisitiza umuhimu wa ushirikiano baina ya wadau wote ili kuhakikisha kuwa mkulima ananufaika ipasavyo na juhudi zake, huku akielekeza kuhakikisha mizani yote inayotumika imethibitishwa na wakala wa vipimo .

“Serikali inataka kuona wakulima wananufaika, na hakuna sababu ya mkulima kudhulumiwa kutokana na uzito usio sahihi au ucheleweshaji wa malipo,” ameongeza Mhe. Masindi.

Ameyakumbusha makampuni yanayodaiwa na Halmashauri hiyo madeni ya misimu iliyopita kulipa fedha hizo hadi ifikapo ijumaa Mei 16 mwaka huu tofauti na hapo makampuni hayo hayataruhusiwa kununua pamba Wilayani humo kwa msimu mpya wa 2025/2026.

Katibu Tawala Wilayani Kishapu Fatma Mohamed amewataka maafisa ugani kuendelea kutoa elimu kwa wakulima na wavunaji wa pamba kuzingatia kanuni za ubora ili pamba yao isichafuke huku wakitakiwa kuhifadhi kwenye mashuka ama nguo na sio mifuko isiyoruhusiwa.

Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri David Mashauri amesema serikali inayompango wa dhati kuhakikisha mkulima ananufaika na makampuni ambayo hayajaomba maeneo ya kununua pamba waje kwa wingi na serikali itawapa maeneo ya uwekezaji.

Kikao hicho ni sehemu ya jitihada za Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu katika kuimarisha sekta ya kilimo na kuhakikisha kuwa zao la pamba linaendelea kuwa chanzo kikuu cha uchumi kwa wakazi wa eneo hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe.Peter Masindi akizungunza kwenye kikao cha Kujadili maandalizi ya ununuzi wa pamba msimu mpya wa mwaka 2025/2026 katika ukumbi wa Shirecu Mei,14,2025 kilichowakutanisha na wadau mbalimbali wa zao la pamba.
Mratibu wa pamba Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Richard Mangua akizungumza kwenye kikao cha Kujadili maandalizi ya ununuzi wa pamba msimu mpya wa mwaka 2025/2026 katika ukumbi wa Shirecu Mei,14,2025.
Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga David Mashauri akizungumza kwenye kikao cha Kujadili maandalizi ya ununuzi wa pamba msimu mpya wa mwaka 2025/2026 katika ukumbi wa Shirecu Mei,14,2025.
Katibu Tawala Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Fatma Mohamed akizungumza kwenye kikao cha Kujadili maandalizi ya ununuzi wa pamba msimu mpya wa mwaka 2025/2026 katika ukumbi wa Shirecu Mei,14,2025.
Mkaguzi wa pamba Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Benson Mhimba akielezea kanuni na sheria mbalimbali za bodi ya pamba kwenye kikao cha Kujadili maandalizi ya ununuzi wa pamba msimu mpya wa mwaka 2025/2026 katika ukumbi wa Shirecu Mei,14,2025.
Afisa biashara Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Ezekiel Alphonce akielezea sheria mbalimbali zinazohusu masuala ya leseni za biashara kwenye kikao cha Kujadili maandalizi ya ununuzi wa pamba msimu mpya wa mwaka 2025/2026 katika ukumbi wa Shirecu Mei,14,2025.
Mwanasheria wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Benard Kadanga akichanganua sheria mbalimbali zinazohusu masuala ya mikataba ya ununuzi kati ya Halmashauri na makampuni kwenye kikao cha Kujadili maandalizi ya ununuzi wa pamba msimu mpya wa mwaka 2025/2026 katika ukumbi wa Shirecu Mei,14,2025.
Mwakilishi wa Meneja wa Shirecu Asnath Changamike akizungumza kwenye kikao cha Kujadili maandalizi ya ununuzi wa pamba msimu mpya wa mwaka 2025/2026 katika ukumbi wa Shirecu Mei,14,2025 kilichowakutanisha wadau mbalimbali wa pamba, ofisi ya Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi Mtendaji.
Mkuu wa Jeshi la zimamoto na uokoaji Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga A/INSP Masoud Mwagilo akitoa elimu ya moto kwenye kikao cha kujadili maandalizi ya ununuzi wa pamba msimu mpya wa mwaka 2025/2026 katika ukumbi wa Shirecu Mei,14,2025 kikiwakutanisha wadau mbalimbali wa pamba, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi Wilayani humo.

By Mpekuzi

Post a Comment

Previous Post Next Post