
Na Regina Ndumbaro Masasi-Mtwara
Mkuu wa Wilaya ya Masasi, Mheshimiwa Rachel Kasanda, ameshiriki kikao maalum cha kuvunjwa kwa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Mji Masasi kilichofanyika hivi karibuni, ambapo amewapongeza madiwani wote kwa kazi nzuri na ya kizalendo waliyofanya katika kipindi cha miaka mitano ya uongozi wao.
Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Masasi, Ndugu Prosper, ametumia fursa hiyo kulishukuru Baraza hilo kwa mchango mkubwa walioutoa katika kuleta maendeleo ya halmashauri.
Ameeleza kuwa kupitia ushirikiano wa pamoja kati ya madiwani na watendaji, halmashauri imeweza kutekeleza miradi mingi ya kimkakati kwa mafanikio makubwa.
Diwani wa Kata ya Nyasa, Mheshimiwa Mbaraka Kodo, amewashukuru wananchi wa kata yake kwa kuwa bega kwa bega naye katika kipindi chote cha miaka mitano.
Ameeleza kuwa ushirikiano huo ndio uliomuwezesha kuwawakilisha wananchi kwa ufanisi na kusukuma mbele ajenda za maendeleo kwa mafanikio makubwa.
Kikao hicho cha kuvunjwa kwa Baraza ni sehemu ya mchakato wa kuhitimisha muhula wa uongozi wa madiwani wa kipindi cha 2020-2025, ambapo viongozi mbalimbali wametumia fursa hiyo kutoa salamu za pongezi na shukrani kwa utumishi uliotukuka kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wa Masasi Mji.
By Mpekuzi
Post a Comment