MASHINDANO YA SAMIA CUP MKINGA YAFANA, MSHINDI AJINYAKULIA SH M. 5 TASLIMU |Shamteeblog.


Na Hamida Kamchalla, MKINGA.

MEELEZWA kwamba michezo hasa mpira wa miguu ni ajira kwa vijana lakini pia huwatoa vijana hao kwenye vijiwe na kuwafanya watambue nafasi na wajibu wao katika jamii zao ambapo kwa upande mwengine wanaweza kuoneana katika timu kubwa.

Mkurugenzi wa Makampuni ya Duvii Farms na Duvii Transport Saidi Rashid Duvii ameyasema hayo wakati wa fainali ya Kombe la Samia Cup Mkinga, katika Wilaya ya Mkinga ambapo timu  zilishiriki na hatimaye timu ya Chafupozi kuibuka kidedea kwa magoli mawili ya penati kwa moja dhidi ya timu ya Kasera.

Mkurugenzi huyo ambaye ni mdau mkubwa wa maendeleo amesema katika juhudi za kuunga serikali mkono katika michezo ameandaa mashindano hayo ikiwa ni sambamba na kurudisha fafhila kwa wananchi wilayani humo kupitia makampuni yake.

"Tumeanzisha ligi hii kwasababu pia asilimia kubwa ya vijana wapo mtaani, hivyo kwa kufanya hivi vijana hawa wataweza kuonekana lakini pia kuweza kupata ajira na kujiajiri, kuna vipaji vingi sana vinaishia mashambani, hivyo tumefanya ligi hii ili kuwaonesha watu kwamba vipaji vipo huku" amesema.
Sambamba na hayo, mkurugenzi huyo amebainisha kwamba mashindano hayo yatakuwa ni muendelezo ikiwa ni kuwaletea vijana pamoja na kujenga umoja na mdhilamano baina yao.

Naye aliyekuwa mwenyekiti wa timu ya Coastal Union ya jijini Tanga Ahmed Aurora amesema moja ya lengo la mashindano hayo ni pamoja na kusaka vipaji ambapo pia yatasaidia kupata timu ambayo itakuwa ya kudumu wilayani humo.

"Sasa kupitia mashindano haya, tunakwenda kutengeneza timu moja ambayo naamini itakuwa bora kabisa ambayo itakwenda kushiriki katika ligi kuanzia chini hadi juu na kwa kuanza tayari tumeshapata vipaji hivyo" amebainisha Aurora.

Katika mashindano hayo, mshindi wa kwanza amezawadiwa Kombe, pesa taslimu shilingi Milioni 5 na medali, mshindi wa pili amepewa sh Milioni 3 na medali, mshindi wa tatu amepata shilingi Milioni 2 na wa nne shilingi Milioni 1.


By Mpekuzi

Post a Comment

Previous Post Next Post