Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe.Peter Masindi akikabidhi hati milki ya kimila kwa wananchi wa Kijiji cha mfano cha Idukilo Kata ya Idukilo Wilayani humo Julai 23,2025 wakiwa ni miongoni mwanufaika wa Vijiji 16 vinavyozunguka migodi ya Williamson na Al hilali kwenye mpango wa Tume ya taifa ya mpango wa Matumizi ya ardhi
Na Sumai Salum – Kishapu
Wananchi 1,200 kutoka Vijiji vya Mwaduhi Lohumbo na Idukilo, Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga, wamekabidhiwa hati za kimila zinazowapa haki halali ya umiliki wa ardhi, hatua inayotarajiwa kuboresha maisha yao kijamii na kiuchumi.
Zoezi hilo ni sehemu ya mpango wa matumizi bora ya ardhi unaosimamiwa na Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi, ambapo vijiji 16 vinavyozunguka mgodi wa Williamson na Al hilal na kutengwa vijiji viwili vya mfano ikiwa ni pamoja na Idukilo na Mwaduhi Lohumbo.
Hati hizo zimekabidhiwa kwa wananchi Julai 23, 2025 na Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Peter Masindi ambaye amesisitiza umuhimu wa hati hizo na matumizi yake sahihi kwa maendeleo ya wananchi.
Akizungumza na wananchi wakati wa makabidhiano hayo, Mhe. Masindi amesema kuwa hati hizo zimetolewa bure chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, hivyo wananchi wanapaswa kuzihifadhi vizuri na kuzingatia thamani yake.
"Serikali ya Mhe. Samia imewapa hati ambazo hamjazigharamikia chochote. Huu ni urithi wa thamani. Mtu asiye na umiliki wa ardhi anadharaulika; ardhi yenye thamani ni ile inayotambulika kisheria,” amesema Mhe. Masindi.
Amehimiza pia matumizi ya hati hizo kama dhamana za kupata mikopo kwenye taasisi za kifedha, jambo ambalo linaweza kuibua fursa za biashara, kilimo cha kisasa na kuimarisha uchumi wa familia na jamii
Akihimiza kasi ya utekelezaji wa mpango huo, Mhe. Masindi amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kishapu Emmanuel Johnson kuhakikisha Vijiji vilivyobakia kati ya 16 vinaingizwa kwenye mpango wa matumizi bora ya ardhi.
Kwa upande wake, Mratibu wa zoezi hilo kutoka Tume ya Matumizi ya Ardhi Edward Mpanda amesema mwitikio wa wananchi umekuwa mkubwa huku wengi wakionesha hamasa ya kutaka mpango huo kuendelezwa zaidi.
“Mwanzoni kulikuwa na changamoto ya mwamko, lakini baada ya elimu kutolewa na wananchi kuelewa faida zake, tumeshuhudia ushiriki mkubwa,tunaishukuru Serikali na uongozi wa Wilaya kwa kuipa kipaumbele haki ya ardhi kwa kila mwananchi,” amesema Mpanda.
Mkurugenzi wa Halmashauri Emmanuel Johnson ametoa wito kwa wananchi kutambua thamani ya mipango waliyoiweka katika matumizi ya ardhi, akisisitiza umuhimu wa kutovamia maeneo yaliyotengwa kwa matumizi ya umma.
“Wananchi mheshimu mipango yenu msivamie maeneo ya huduma kama shule, zahanati au Barabara hata makaburi na masoko,badala yake tumieni muda wenu mwingi kufanya shughuli za maendeleo na kiuchumi,” amesema Johnson.
Baadhi ya wananchi walionufaika na hati hizo wamesema hatua hiyo ni ukombozi mkubwa huku Anna Elikana kutoka Kijiji cha Idukilo amesema kuwa hati hiyo italinda familia yake dhidi ya migogoro ya ardhi, hasa kati ya wake kwa waume.
“Wanaume wamekuwa wakiuza viwanja bila kuwashirikisha wake zao sasa tuna nyaraka halali, tuko salama,” amesema Anna kwa furaha.
Zabron Kulwa kutoka Kijiji cha Mwadui Lohumbo ameongeza kuwa mpango huu umekuwa mkombozi wa wanawake na watoto, ambao mara nyingi wamekuwa waathirika wa migogoro ya ardhi na unyanyasaji wa mali huku wakijikwamua kiuchumu kwa kupata elimu ya mikopo.
Hatua ya serikali kutoa hati 1,200 za kimila Wilayani Kishapu si tu ishara ya dhamira ya serikali katika kulinda haki za ardhi kwa wananchi na kuondoa migogoro ya ardhi, bali pia ni kichocheo cha maendeleo ya kiuchumi, kijamii na kijinsia.
Mpango huu unatoa dira ya matumaini kwa maelfu ya wananchi wanaotegemea ardhi kama msingi wa maisha yao ikiwa na maana kuwa maendeleo ya kweli yanaanzia na umiliki halali wa rasilimali.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe. Peter Masindi akizungumza wakati akikabidhi hati za kimila kwenye Vijiji viwili vya mfano vya Mwadui Lohumbo na Idukilo kati ya Vijiji 16 vilivyokuwa kwenye mpango wa matumizi ya ardhi Julai 23,2015
Mratibu wa mradi kutoka Tume ya taifa ya mpango wa matumizi ya ardhi Edward Mpanda akizungumza wakati Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe Peter Masindi alipokuwa akikabidhi hati za kimila kwa wananchi wa Vijiji viwili vya mfano Mwadui Lohumbo na Idukilo kati ya Vijiji 16 vilivyokuwa kwenye mradi wa mpango wa matumizi ya ardhi Julai 23,2015
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Emmanuel Johnson akizungumza wakati Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe.Perer Masindi akikabidhi hatimilki za kimila kwa wananchi wa Vijiji viwili vya mfano Mwadui Lohumbo na Idukilo kati ya Vijiji 16 vilivyokuwa kwenye mradi wa mpango wa matumizi ya ardhi Julai 23,2015

Mtendaji wa Kata ya Mwadui Lohumbo Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Juma H.Juma akizungumza kwenye makabidhiano hayo

Mtendaji wa Kata ya Idukilo Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Enock Manyenye akizungumza kwenye makabidhino hayo

Mwenyekiti wa Kijiji cha Mwaduhi Lohumbo Kata ya Mwadui Lohumbo Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Joseph Jisena akifungua mkutano maalumu wa ukabidhiwaji hatimilki za kimila kwa wananchi Julai 23,2025

Mwenyekiti wa Kijiji cha Idukilo Kata ya Idukilo Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Patrick Kapele akifungua mkutano maalumu wa ukabidhiwaji hatimilki za kimila kwa wananchi Julai 23,2025

Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe.Peter Masindi(Kushoto) na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Emmanuel Johnson (kulia) wakifurahi kwa pamoja na kupeana mikono ya pongezi kwa serikali ya awamu ya sita kwa kuwasogezea wananchi huduma za msingi bila kuwatoza gharama walipokuwa kwenye zoezi la ugawaji hati milki ya kimila uliortibiwa na serikali kupitia Tume ya taifa ya mpango wa matumizi ya ardhi kijiji cha Mwadui Lohumbo na Idukilo Wilayani Humo Julai 23,2025

By Mpekuzi
Post a Comment