Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, SACP Janeth MagomiNa Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Akizungumza na vyombo vya habari leo Julai 23, 2025, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, SACP Janeth Magomi, amesema operesheni hizo zimehusisha ukamataji wa watuhumiwa wa makosa ya kutumia na kusambaza dawa za kulevya pamoja na wizi wa mali mbalimbali.
Katika operesheni hizo, dawa za kulevya zilizokamatwa ni pamoja na bhangi gramu 226.1, mirungi kilo 2.96, pamoja na pombe ya moshi lita 142.
Aidha, vitu vingine vilivyokamatwa ni pikipiki 2, mabati 16, nondo vipande 17, vitanda 4, redio 08, bajaji 01, na risasi moja ya silaha ndogo.
Kamanda Magomi amesema kuwa operesheni hizo zinaendelea kwa lengo la kuhakikisha jamii inakuwa salama dhidi ya vitendo vya uhalifu na matumizi ya dawa za kulevya.
Amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za wahalifu na vitendo viovu vinavyofanyika katika maeneo yao.
By Mpekuzi
Post a Comment