
Santiel Erick Kirumba (kulia) na Dkt. Christina Christopher Mnzava

Santiel Erick Kirumba (kushoto) na Dkt. Christina Christopher Mnzava - (Picha kutoka Maktaba ya Malunde Media)
Na Mwandishi wetu - Malunde 1 blog
Mkutano Mkuu Maalum wa uchaguzi wa wagombea wa Ubunge wa Viti Maalum kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa Mkoa wa Shinyanga umefanyika kwa mafanikio makubwa leo katika ukumbi wa Shule ya Wasichana Shinyanga, ukishuhudia wagombea wawili wakiongoza kwa kishindo.
Katika mchakato huo uliovuta hisia za wanachama wengi, wajumbe 1,036 kutoka Wilaya za Shinyanga Mjini (133), Kahama (440), na Kishapu (227) wamepiga kura kuwachagua wanawake wawili kati ya wagombea wanane waliokuwa wakisaka nafasi hizo.
Santiel Erick Kirumba ameibuka kinara kwa kura 730, akifuatiwa kwa karibu na Dkt. Christina Christopher Mnzava aliyepata kura 719, na hivyo kufanikiwa kuibuka washindi wa nafasi hizo mbili muhimu kwa Mkoa wa Shinyanga.
Katika mchuano huo uliokuwa na mvutano mkubwa wa kisiasa, wagombea wengine waliojitokeza lakini hawakufanikiwa kuingia nafasi mbili za juu ni pamoja na Salome Wycliffe Makamba aliyepata kura 216 na Mwanahamis Munkunda aliyepata kura 196.
Wengine ni Felister Wilson Buzuka aliyepata kura 34, Alice Salvatory Kyanila (kura 29), Christina Kija Gule (kura 23) na Queenelizabeth William Makune aliyepata kura 19.
Kwa ushindi huo wa kura za maoni, Santiel Kirumba na Dkt. Christina Mnzava ni washindi katika uchaguzi huo nafasi ya Ubunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga.





























By Mpekuzi
Post a Comment