Mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee, Watoto na Vijana Bi. Anna Mathias Paul (ushungi wa njano) pamoja wageni waalikwa.
Mkurugenzi wa Taasisi ya mama Taifa, Bi. Neema Karume
Kaimu Katibu wa Taasisi Bw. Ibrahim Minga Elias
Mkurugenzi wa Taasisi ya mtetezi wa mama Kanda ya Zanzibar, Bi. Chausiku Mohamed Hamisi
Afisa uhusiano wa Taasisi ya mtetezi wa mama Bw. Twaha Twalib
Mwenyekiti wa Taasisi mkoa wa Mbeya Bi. Tumsuume Mwakinyuki
Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan


NA. ELISANTE KINDULU, ZANZIBAR
MKURUGENZI wa Taasisi ya Mtetezi wa mama ngazi ya Taifa Bi. Neema Karume amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi kwa kuleta maendeleo hasa katika kipindi hiki cha miaka mitano iliyopita.
Bi. Neema ameyasema hayo jana alipokuwa akimkaribisha Naibu waziri wa Maendelea ya jamii, jinsia,wazee, watoto na vijana Mh. Anna Athanas Paul ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla fupi ya uzinduzi wa Taasisi hiyo Kanda ya Zanzibar.
Bi. Neema amesema kutokana na maendeleo ya ujenzi wa barabara, vituo vya afya, shule na huduma mbalimbali za kijamii na kiuchumi viongozi hao hawana budi kuungwa mkono katika juhudi za kuwaletea wananchi maendeleo.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia,wazee,watoto na Vijana Mh. Anna Athanas Paul aliitaka taasisi hiyo kuhakikisha wanapunguza au kutokomeza mmomonyoko wa maadili unaoshamili kwa sasa katika familia zetu.
Naibu waziri huyo alisema wizara yake chini ya Waziri Mh. Riziki Pembe watakuwa bega kwa bega kusaidia huduma mbalimbali zitakazohitajika na taasisi hiyo ikiwemo changamoto ya ofisi na vitendea kazi kwa kanda ya Zanzibar kwa kuwa wizara na taasisi wote kwa pamoja wana lengo la kumhudumia mama na mtoto bila kumsahau baba.
"Wanawake wengi na watoto wanadhalilishwa. Wakina baba wao wanajificha sisi hatujui. Mkipigwa semeni tuweze kuleta suluhu kwenye familia ili hata watoto wawe na amani",alisema naibu waziri.
Aidha Mh. Anna aliitaka taasisi hiyo kuhamasisha wananchi kupitia vyombo mbalimbali vya Habari ikiwemo mitandao ya kijamii kuhimiza uchaguzi wa kistaarabu na wa amani ili kupata viongozi walio chaguo la wananchi.
"Nendeni mkawasemee Dkt. Samia na Dkt Mwinyi kwenye mitandao na kupita media mbalimbali bila matusi. Viongozi wetu awamu hii wameupiga mwingi sana hadi kupitiliza kutokana na Ilani. Hivyo hakuna ugumu wa kuwapa mitano tena",alisema naibu waziri.
Katika risala yake, Katibu wa Taasisi ya mtetezi wa mama Kanda ya Zanzibar, Bw. Abubakar Halfan Zahoro alizitaja changamoto kadhaa katika taasisi hiyo Kanda ya Zanzibar kuwa ni ukosefu wa ofisi ,vitendea kazi na ufinyu wa rasilimali fedha.
Uzinduzi huo ambao ulitanguliwa na ziara ya utalii katika kisiwa hicho ulihudhuria na viongozi na wanachama wa taasisi hiyo kutoka mikoa ya Tanzania Bara na Visiwani.
Viongozi wengine walioshiriki katika uzinduzi huo ni pamoja na Mkuu wa wilaya ya mjini Mohamed ally, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Dimani Bw. Ali Mjema, Mkurugenzi wa taasisi hiyo kanda ya Zanzibar Bi.Chausiku Mohamed Hamisi , Afisa wa Taasisi anayeshughulikia TEHAMA Bw. Edward Nswima na Diwani wa kata ya Dimani Mh. Farashuu Abdalla.
By Mpekuzi












Post a Comment